Asaidia mabadilishano kati ya China na Kenya kwa kutegemea nguvu yake ya kujua kuongea kwa lugha mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 09, 2022

Kituo cha Port Reitz kiko kwenye bandari ya Mombasa, mashariki ya Kenya, ni kituo cha kwanza cha Reli ya Mombasa-Nairobi. Hesbon Aginga mwenye umri wa miaka 29 akiwa naibu mkuu wa kituo hicho anashughulikia zaidi kazi ya usafirishaji wa bidhaa kwenye njia ya reli. Zaidi ya hayo, pia ana kazi muhimu ya kama daraja la mawasiliano kati ya mafundi wa reli wa China na wafanyakazi wa Kenya.

Tangu Reli ya Mombasa-Nairobi ulipoanza kujengwa mwaka 2014, mawasiliano kati ya wafanyakazi wa China na wa Kenya yalikutana na tatizo kubwa. Awali, wafanyakazi walifanya mawasiliano kwa kutegemea app ya tafsiri, hata kutegemea lugha ya ishara. Hesbon Aginga anayejua kuongea lugha ya Kichina na Kiingereza anasaidia kupunguza sana tatizo hilo.

Hesbon Aginga (kati) na wenzake wakikagua hali ya uendeshaji wa chaja. (Picha na Kampuni ya Africa Star)

Alipokuwa mtoto, Aginga alikuwa anatamani kusoma lugha ya kigeni. Alisoma somo la lugha ya Kichina kwa miezi mitatu kwenye Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Nairobi, baadaye kutokana na alama zake nzuri,alipendekezwa kwenda Chuo Kikuu cha Uwalimu cha Harbin nchini China kuendelea na masomo kwa mwaka mmoja. Baada ya kurudi Kenya, Akinga alikuwa Mkenya wa kwanza kufanya kazi katika Kituo cha Port Reitz kutokana na nguvu yake bora ya lugha.

Mwanzoni alijua kidogo juu ya uendeshaji wa reli, lakini kwa kutegemea shauku yake na juhudi zake, pamoja na kujua kuongea kwa lugha ya Kichina, siku hadi siku alipata ujuzi wa usimamizi wa reli, usalama wa moto na ujuzi mwingine unaohusiana, amekuwa naibu mkuu wa kituo cha Port Reitz kutoka sekretari, ambaye anasimamia wafanyakazi 42. "Sikutarajia kuwa ningekuwa mfanyakazi wa reli niliposoma lugha ya Kichina. Lugha hiyo imeniletea fursa nyingi." Mwezi Septemba, 2021, Akinga pia alishiriki kwenye semina iliyofanyika kwenye mtandao wa intaneti kuhusu uendeshaji na usimamizi wa Reli ya Kenya, semina hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya China iliendeshwa na Chuo Kikuu cha Usafirishaji cha Beijing. Alisema masomo kwenye semina yalimwongezea ujuzi kuhusu uendeshaji na usimamizi wa reli. 

Hesborn Aginga (kati) na wenzake wakifanya kazi katika ofisi ya usimamizi wa treni. (Picha na Kampuni ya Africa Star)

Hesbon Aginga ni Mkenya pekee anayejua kuongea kwa lugha ya Kichina katika Kituo cha Port Reitz. Kila mafundi wa China wanapotoa mafunzo na kufanya mazoezi, Aginga anahitaji kuwafuata kwenda mahali pa ujenzi wa mradi, ambapo anatoa ufafanuzi kwa Kichina juu ya maana ya kila dhana kwa kufuata mafunzo ya mafundi wa China.

Aginga hufundisha wenzake na familia yake kuongea kwa lugha ya Kichina wakati wa mapumziko. “Watu wote wana hamu kubwa juu ya lugha ya Kichina, mara kwa mara wanaweza kuniuliza namna ya kuvitaja kwa Kichina vitu vilivyoko karibu nao. ”

Hesborn Aginga (wa kwanza kulia) akiwaelekeza wafanyakazi jinsi ya kufunga vifaa vya ulinzi nyuma ya treni. (Picha na Kampuni ya Africa Star)

Wakati akipata nafasi Akinga huenda Kituo cha magharibi cha Mombasa kilichoko karibu na ofisini kwake huwasaidia watalii wa China waliopata tatizo la kuongea. "Wachina wengi hawajui jinsi ya kuchapisha tikiti ya treni katika kituo baada ya kununua tikiti mtandaoni, wakati huo naenda kuwasaidia." Siku za kawaida, kama akikutana na Wachina wasiojua kuwasiliana vizuri na wakenya kwa sababu ya lugha , pia anawasaidia kwa hiari. Alisema, kutokana na hayo amepata marafiki wengi wa China.

Akizungumzia mpango wake wa ajira katika siku za baadaye, Akinga ana matumaini ya kuendelea kuboresha kiwango chake cha kazi, kusaidia Wakenya wengi zaidi kujifunza ujuzi kuhusu reli, na kuchangia kwa maendeleo ya Reli ya Mombasa-Nairobi na nchi yake.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha