Hadithi yenye ajabu ya Yasef Ananda katika Dora kubwa ya Tang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 09, 2022

Watu wengi walisema mara kwa mara kuwa, “Mji wa Chang'an (uliokuwa Mji Mkuu wa China katika Enzi ya Tang) ni mji mkubwa, lakini hawajui katika mitaa ya Mji wa Chang'an kulikuwa na hali motomoto ya namna gani. Sasa, Bw. Yasef kutoka Cuba “anapita” Mji wa Chang'an, akisoma mashairi pamoja na “Li Bai”(aliyekuwa mshairi maarufu katika Enzi ya Tang), na kuonja chakula kitamu mjini humo. Hebu tufuate kamera kwenda Mji wa Xi’an, Mkoa wa Shaanxi na “kujionea” maisha ya watu wa Mji wa Chang’an wa zama za kale.

“Saa 12 za Chang'an” ni jina la mtaa wa kwanza unaoonesha mitindo ya maisha ya watu katika Enzi ya Tang ya China katika zama za kale, ambapo watu wanaweza“kujionea”maisha ya watu wa Enzi ya Tang.

Katika mtaa wa “Saa 12 za Chang'an”, kuna “njia 12 za Chang'an”, "vitoweo 12 maarufu", "maonyesho 12 ya michezo ya sanaa " na "sherehe 12 za sikukuu za Enzi ya Tang", yote hayo yameonesha vilivyo hali mbalimbali za kuwavutia watu katika dola kubwa ya Tang wakati wa zama za kale za China. Katika mtaa wa “Saa 12 za Chang'an” watalii wanaweza “kujionea” vilivyo mvuto wa Enzi ya Tang, na wakihisi kama wamekuwa watu wanaoishi katika Enzi ya Tang na kujiburudisha kwa furaha.

Bw. Yasef alipata kumbukumbu nyingi katika safari yake hiyo maalum, akisema mtaa huo ni wa kipekee sana, ni tofauti na mahali popote alipakwenda hapo kabla, ambapo aliona kama kweli alipita mtaa uliokuwa wa Enzi ya Tang ya zama za kale, na pia alijionea mambo ya kisasa ya China mpya. Alisema: "Niliona watu wa familia nyingi, watoto na wazee waliokuja kutembelea kwenye mtaa huo na kufurahia hali ilivyo kama ya kihalisi ya maisha ya watu katika Enzi ya Tang." Anawashauri wageni wanaoishi nchiniChina na ng’ambo pia watatembelea mtaa huo na kuhisi mvuto wa huko, alisema mtaa huo kweli ni mahali maalum penye miujiza na kuvutia sana.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha