“Ni bora kumfundisha mtu kuvua samaki kuliko kumpa samaki.” Mwalimu wa China na mwanafunzi wake wa Kenya wajenga pamoja Reli ya Mombasa-Nairobi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 10, 2022

Kuzinduliwa rasmi kwa Reli ya Mombasa-Nairobi kumetoa nafasi nyingi za ajira na fursa ya kujifunza ufundi. China imeisaidia Kenya kuwaandaa wafanyakazi zaidi ya 1,700 wenye ufundi wa kazi na usimamizi wa reli, na imeanzisha kituo cha mafunzo ya kuwaandaa wataalamu na chuo cha teknolojia ya reli nchini Kenya ili kuisaidia Kenya kuboresha uwezo wake wa kujiendeleza.

Mkuu wa eneo la kazi ya kiderenge kwenye Reli ya Mombasa-Nairobi Bw. Heng Lei anabeba wajibu wa kutoa mafunzo ya ufundi wa kiderenge, mpaka sasa amewafundisha wanafunzi wengi wa China na wa Kenya, John Oketch ni mmoja kati yao.

Heng Lei akimwelekeza John Oketch kupima sehemu za treni ziko sawa au la.(Picha na Kampuni ya Africa Star)

Kabla ya kuendesha gari la usimamizi wa reli , Heng Lei na John Okeqi wakithibitisha pamoja hali ya kwenye njia ya reli. (Picha na Kampuni ya Africa Star)

Kabla ya John Oketch kufanya kazi kuhusu mradi wa reli ya Mombasa-Nairobi, alikuwa hana ujuzi wa reli na treni hata kidogo. "Reli ya Mombasa-Nairobi imebadilisha maisha yangu, na kuniwezesha kulisha familia yangu na kuinua kiwango changu cha kazi. Ninashukuru sana mabadiliko na nafasi za kazi zinazoletwa na ujenzi wa reli hii i kwa watu wa Kenya." Okech alisema kwa dhati.

“Nimewafundisha wanafunzi zaidi ya 20, Oketch anasoma na kufanya kazi kwa makini sana, akipata tatizo aliniuliza, yeye ni mwanafunzi wangu mzuri. ”Heng Lei alipotaja Oketch alijivunia sana. "Wanafunzi ambao nimewafundisha wote ni hodari, na wanaonekana kuwa wanapenda sana kazi ya reli," Heng Lei alisema.

“Ni bora kumfundisha mtu kuvua samaki kuliko kumpa samaki. " “Ufundi kuhusu kiderenge ni ufundi mpya nchini Kenya, Mwalimu Heng alinifundisha ujuzi na ufundi mwingi, na amenishawishia vizuri namna ya kusimamia muda na kutumia muda kwa ufanisi.” Kuwa dereva wa kuendesha kiderenge kufanya usimamizi kwenye njia ya reli kutoka mtu asiyejua ufundi wa kazi, Oketch alisema mara kwa mara kuwa anashukuru sana msaada usio na binafsi kutoka kwa mwalimu wake wa China. 

John Oketch akiendesha gari la usimamizi wa reli pekee yake.(Picha na Kampuni ya Africa Star)

Muonekano wa mahojiano. (Mpiga picha: Yu Yang)

Tangu Heng Lei ashiriki kwenye ujenzi wa mradi wa Reli ya Mombasa-Nairobi, alirudi China kujumuika pamoja na familia yake mara tatu tu. “Kuna msemo mmoja ‘Acha familia ndogo, wasaidie watu wote ’, ningependa kushiriki kwenye ujenzi wa mradi wa Reli ya Mombasa-Nairobi na kutoa mchango wangu mdogo kwa ajili ya ujenzi wa ‘Ukanda Mmoja na Njia Moja’ na ninaamini familia yangu itajivunia kwa mimi."

Urafiki kati ya mwalimu wa China na mwanafunzi wa Kenya katika ujenzi wa Reli ya Mombasa-Nairobi unaonesha ushirikiano kati ya China na Kenya unaoendelezwa kwa kina na kupata mafanikio halisi. Katika miaka mitano iliyopita, chini ya pendekezo la “Ukanda Mmoja na Njia Moja”, China inategemea nguvu yake ya ufundi kusaidia Kenya kuwaandaa wataalam na kuendeleza teknolojia, na reli hiyo imekuwa njia inayounganisha ustaarabu wa China na wa Afrika. Watu wa China na Afrika watashikana mikono ili kuelekea siku zenye mustakabali mwema zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha