Hatua za dharua na kutegemeka zahitajiwa kwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 15, 2022

Tarehe 14, Agosti, 2022, wahudumu waliojitolewa wakipeleka sampuli za upimaji wa virusi vya korona huko Sanya, Mkoa wa Hainan, China. (Picha/Xinhua)

Naibu waziri mkuu wa China Sun Chunlan alisisitiza kuwa, kazi ya kudhibiti kwa haraka na ya kutegemeka dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona inapaswa kufanyika kwenye Mkoa wa Hainan, ili kutimiza maambukizi sifuri katika jamii kwa haraka iwezekanavyo, kuhakikisha afya na usalama wa umma, na kurudisha hali ya kawaida ya maisha na uzalishaji.

Sun alisema hayo alipokagua kazi ya kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona huko Sanya, mji maalum wa utalii wa mkoa wa Hainan, China, ambapo ni kiini cha maambukizi hayo ya Kisiwa cha Hainan kuanzia tarehe 1, Agosti. Kamati ya Afya ya Mkoa huo Jumapili ilisema, kwa jumla idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya korona iliongezeka hadi 3,000 na idadi ya watu walioambukizwa virusi bila ya dalili imeongezeka hadi 3544 mjini kote mpaka Jumamosi.

Maambukizi ya virusi vya korona yaliwafanya watalii 150,000 wakwame huko. Hadi Jumapili saa 12 asubuhi, usafiri 14,247 wa ndege umepangwa kwa ajili ya kuwasaidia watalii hao kurudi Shanghai, Beijing, Tianjin na miji mingine kadha wa kadha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha