Milango mipya imefunguliwa kwa watu wenye tatizo la kuona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 16, 2022

Wanafunzi wasioona walisoma vitabu vya hati nundu katika maktaba ya shule ya elimu maalum huko Haikou, mkoa wa Hainan. [Picha na KANG DENGLIN/FOR CHINA DAILY]

Mamilioni ya vitabu vipatikana kwa walemavu wa macho

Yin Menglan mwenye umri wa miaka 33 ni mlemavu wa macho ambaye amekuwa mhakiki katika Shirika la Uchapishaji wa vitabu vya hati nundu la China (CBP) kwa miaka 11, na kufanya kazi kwa kugusa ubao wa hati nundu unaounganishwa na kompyuta.

Kompyuta inabadilisha maandishi ya Kichina kuwa hati nundu. Yin anasoma hati nundu, huku Zhang Chuyi, mtu anayeweza kuona, analinganisha yale aliyosoma Yin na maandishi ya Kichina, ambapo wanasahihisha makosa kwenye kompyuta.

Yin ni mmoja wa zaidi ya wahakiki kumi katika shirika hilo ambao husaidia uchapishaji wa vitabu vya hati nundu .

Mwezi Mei, China ilijiunga rasmi na Mkataba wa Marrakesh wa Kuleta urahisi kwa watu wasioona au wenye tatizo la kuona katika kusoma vitabu vilivyochapishwa, kwa ufupi unaoitwa Mkataba wa Marrakesh.

Mkataba huo unazitaka nchi zilisaini mkataba huo kutoa kanuni na ruhusa maalum katika kanuni za hakimiliki ya unakili ili kuleta urahisi kwa watu wasioona au wenye tatizo la kuona katika kusoma vitabu vya hati nundu.

Mkataba huo ni habari nzuri sana kwa watu milioni 17 wenye tatizo la kuona nchini China, ambao sasa wamekuwa na vitabu vingi zaidi kuchagua.

Wahariri wamekuwa wakichagua vitabu kwa makini. Wo Shuping, naibu mhariri mkuu wa shirika la CBP, alisema: "Kila mwaka tunachagua elfu kadhaa za vitabu kutoka vile vya sokoni na hatimaye kuamua kuchapisha vitabu 1,000 hivi vya hati nundu. Vitabu hivyo vinahusisha mada mbalimbali za siasa , uchumi, muziki, afya na fasihi."

Wo alisema vitabu vilivyochaguliwa na wahariri huwa si vinavyonunuliwa zaidi, lakini ni vile vinavyosaidia watu kupata mtazamo chanya kuhusu maisha na kufuata maadili. "Tunatumai vitabu vyetu vitaendelea kusomwa na watu baada ya kuchapishwa kwake kwa miongo kadhaa," Wo aliongeza. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha