Timu ya Madaktari wa China yatoa huduma za afya bila malipo katika maeneo ya vijiji nchini Cameroon

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2022

Daktari akimpima joto mgonjwa huko Ngat-Bane, Cameroon, Agosti 20, 2022. Timu ya madaktari wa China nchini Cameroon siku ya Jumamosi ilitoa huduma za matibabu bila malipo kwa watu wa Ngat-Bane, kijiji ambacho kiko katika eneo la Centre katika Mji Mkuu, Yaounde. (Picha na Kepseu/Xinhua)

Yaounde - Timu ya madaktari wa China nchini Cameroon siku ya Jumamosi ilitoa huduma za matibabu bila malipo kwa watu wa Kijiji cha Ngat-Bane, katika eneo la Centre la Yaounde, Cameroon.

Mapema asubuhi, wanakijiji zaidi ya mia moja walikusanyika katika Kituo cha Afya cha Ngat-Bane kuwakaribisha madaktari 12 kutoka idara mbalimbali za vipimo vya ultrasound, stomatology, acupuncture, na kadhalika wa timu ya madaktari wa China yenye makao yake huko Mbalmayo, mji ulioko karibu umbali wa kilomita 40 kutoka Yaounde.

Miongoni mwa wanakijiji waliojitokeza kupata huduma ni Richard Mekoga mwenye umri wa miaka 63 ambaye alitoka kijiji jirani. Mekoga alisema alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo na matatizo ya macho na mishipa ya fahamu.

"Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki katika kampeni ya afya ya (Wachina). Nimeridhishwa sana na jinsi tulivyopokelewa," Mekoga alisema, huku akiongeza kuwa ana uhakika kwamba dawa iliyotolewa na timu ya madaktari wa China itamponya.

Kijiji cha Ngat-Bane, kama ilivyo kwa vijiji vingine vingi vya Cameroon, vilivyo pembezoni, kina ukosefu wa hospitali. Wanakijiji mara nyingi wanasumbuliwa na matatizo ya afya kama vile baridi yabisi, homa ya matumbo, na malaria, lakini wengi wao hawawezi kumudu huduma za matibabu huko Mbalmayo.

“Ni mashauriano na matibabu ya bure ya Wachina hutusaidia sisi ambao hatuna uwezo wa kutosha na ambao hatuwezi hata kusafiri kwenda Mbalmayo (kwa matibabu),” anasema Joseph Mbede Onambele mwenye umri wa miaka 70 ambaye alikuwa akisumbuliwa na uvimbe katika miguu na mikono na wakati mwingine husafiri hadi Mbalmayo kupokea matibabu kutoka kwa wahudumu wa afya wa China wanaofanya kazi huko.

Dieudonne Zang Mba Obele, Meya wa Mbalmayo alikadiria kuwa asilimia 70 ya walioshauriana na kutibiwa bila malipo walikuwa wanawake na watoto.

"Naamini huu ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya Cameroon na China. Wahudumu wa afya wa China siyo tu wanatoa huduma kwa hospitali ya wilaya ya Mbalmayo lakini kwa watu maskini zaidi ambao hawawezi kwenda hospitali ya Mbalmayo, wakati mwingine kwa kukosa namna au ukosefu wa miundombinu," Obele anasema.

Kama sehemu ya kampeni, timu ya madaktari wa China pia ilitoa vifaa tiba.

Madaktari wa China wakimkabidhi meya wa Mbalmayo, Dieudonne Zang Mba Obele dawa zilizotolewa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Ngat-Bane, huko Ngat-Bane, Cameroon, Agosti 20, 2022. (Picha na Kepseu/Xinhua)

Mfamasia akimpatia mgonjwa dawa za bila malipo baada ya mashauriano huko Ngat-Bane, Cameroon, Agosti 20, 2022. (Picha na Kepseu/Xinhua)

Mtu huyu akiangalia dawa alizopokea bila malipo baada ya mashauriano na madaktari wa China huko Ngat-Bane, Cameroon, Agosti 20, 2022. (Picha na Kepseu/Xinhua)

Wafamasia wakisambaza dawa bila malipo kwa wagonjwa baada ya mashauriano huko Ngat-Bane, Cameroon, Agosti 20, 2022. (Picha na Kepseu/Xinhua)

Daktari wa China akitoa matibabu ya acupuncture kwa mgonjwa huko Ngat-Bane, Cameroon, Agosti 20, 2022. (Picha na Kepseu/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha