Kazi ya kuzima moto wa misituni katika eneo la Banan, Chongqing imepata mafanikio ya kipindi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2022

Idara ya uenezi ya manispaa ya Eneo la Banan la Mji wa Chongqing ilitoa habari jioni ya Tarehe 24 ikisema kuwa, hadi saa 12 ya Tarehe 24, kutokana na juhudi zilizofanywa ipasavyo na watu wa Mji wa Chongqing na Eneo la Banan, moto wa misituni uliotokea kwenye upande wa kusini wa Eneo la Banan umedhibitiwa kwenye ukanda wa kutengwa na hakuna moto wazi katika upande wa kaskazini. Picha hii ikionesha hali ya kuzima moto na kuokoa maafa . (Picha na Kituo cha Media Jumuishi cha Eneo la Banan)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha