

Lugha Nyingine
Angola yafanya hafla ya mazishi ya rais wa zamani Jose Eduardo dos Santos
Picha kutoka maktaba iliyopigwa Septemba 26, 2017, ikimuonyesha Rais wa zamani wa Angola Jose Eduardo dos Santos (mbele) wakati wa sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Joao Lourenco mjini Luanda, Angola. (Xinhua/Chen Cheng)
LUANDA, - Hafla ya mazishi ya Rais wa zamani wa Angola Jose Eduardo dos Santos imefanyika Jumapili huko Luanda, mji mkuu wa nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Angola Marcy Lopes, ambaye ni msemaji wa kamati ya maandalizi ya mazishi, alisema Jumamosi kuwa angalau wajumbe 21 wa kigeni, wanaowakilishwa katika hadhi ya juu, walitarajiwa kuwasili Angola kushiriki kwenye hafla ya mazishi ya rais huyo wa zamani wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika.
Jose Eduardo dos Santos, aliyeitawala Angola kuanzia Mwaka 1979 hadi 2017, alifariki Julai 8, 2022 akiwa na umri wa miaka 79, huko Barcelona, Hispania, ambako aliishi kwa muda wake mwingi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Kuwasili Angola kwa mwili wa Jose Eduardo dos Santos mnamo Agosti 20 kulimaliza mzozo wa kudai haki za kuzika mwili miongoni mwa wanafamilia uliodumu tangu Julai 8. Mzozo huo uliamriwa kwa mwili huo kukabidhiwa kwa mjane wake Ana Paula dos Santos baada ya mapambano ya kisheria kati ya pande mbili za familia kwenye mahakama, huko Hispania.
Kisha mwili huo ulipelekwa katika makazi ya rais wa zamani huko Luanda, Angola ambako ulikaa hadi Agosti 27.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma