Shughuli za Uwindaji haramu wa vifaru zazidi kuongezeka Namibia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2022

Msemaji wa Wizara ya Mazingira, Misitu na Utalii Romeo Muyunda alisema Jumatano kuwa idadi ya vifaru waliowindwa kiharamu iliongezeka kuwa 48 mwaka huu.

Katika taarifa yake, Muyunda alisema kati ya vifaru hao waliowindwa kiharamu, 32 ni vifaru weusi na 16 ni vifaru weupe.

"Tunakabiliwa na tatizo la kupambana na uwindaji haramu kwa hatua zenye ufanisi. Kama nilivyoeleza hapo awali, uwindaji haramu umekuwa hali ya kawaida katika mashamba binafsi na mashamba ya ulezi wa vifaru weusi. Sasa tunafanya juhudi za kutekeleza hatua mpya ili kukabiliana na hali hiyo." alisema.

Muyunda alisema Vikundi vya Kupambana na Uwindaji Haramu (APU) katika mashamba binafsi viko katika kuimarishwa nguvu, huku polisi na maofisa wa idara ya utekelezaji wa sheria wakisaidia wakulima binafsi katika kufanya upelelezi, kutekeleza sheria na kufanya doria.

Alisema, "pia tutatumia helikopta yetu kufanya doria katika anga ya maeneo yenye shughuli zaidi za uwindaji haramu."

Msemaji huyo pia alisema, "tunaahidi kwa wananchi kuwa wizara yetu itashirikiana na wahusika wa maslahi katika kuhamasisha watu kwa nguvu kubwa ili kuzuia wimbi hili jipya la uwindaji haramu." Aliwataka wananchi kuendelea na tahadhari na kutoa ripoti ya matukio ya uwindaji haramu na vitendo vingine vya uhalifu vinavyohusika na wanyamapori.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha