Kamati ya Umoja wa Mataifa yaeleza wasiwasi mkubwa kuhusu ufikiaji wa huduma za utoaji mimba nchini Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 02, 2022
Kamati ya Umoja wa Mataifa yaeleza wasiwasi mkubwa kuhusu ufikiaji wa huduma za utoaji mimba nchini Marekani
Waandamanaji wakiwa wamekusanyika nje ya Ukumbi wa Jiji la Los Angeles, katikati mwa mji wa Los Angeles, California, Marekani, Juni 25, 2022. (Xinhua)

LONDON – Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Reuters, Kamati ya Umoja wa Mataifa imesema "ilikuwa na wasiwasi mkubwa" kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Marekani wa Mwezi Juni ambao ulihitimisha haki ya kutoa mimba nchini humo.

“Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi ilisema uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Marekani ulikuwa na "athari mbalimbali kwa afya ya kijinsia na uzazi na haki za watu wa rangi na wa jamii za walio wachache, hasa wale walio na kipato cha chini," inasema ripoti hiyo iliyotolewa Jumanne.

“Kamati hiyo yenye wanachama 18 imeitaka Washington kuchukua hatua mahususi kukomesha mashtaka ya jinai dhidi ya wanawake na watoa huduma za utoaji mimba,” ripoti hiyo imesema, ikimnukuu mwanakamati Pansy Tlakula.

Ripoti hiyo imesema kuwa, Chombo hicho cha Umoja wa Mataifa pia kilitoa wito wa kulipwa fidia kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika ikiwa ni sehemu ya juhudi pana za kushughulikia utumwa uliofanyika kwa karne nyingi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha