

Lugha Nyingine
Biashara ya Kidijitali yawa kichocheo cha kukua kwa uchumi katika nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja
Watu wakitembelea banda la Pakistani kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha China wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China Mwaka 2022 (CIFTIS) hapa Beijing, China, Septemba 3, 2022. (Xinhua/Zhang Fan)
BEIJING - Maelfu ya miaka iliyopita, katika China ya zama za kale, wafanyabiashara walisafiri kwenye njia ya hariri kwa kutumia ngamia na farasi, wakishinda ugumu ili kuuza hariri, chai na utaalam mwingine kutoka China huko Magharibi, wakati huo huo wakiagiza bidhaa za vioo, lulu, matunda na mbogamboga kutoka nje.
Sasa, katika chumba cha utangazaji wa moja kwa moja kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China Mwaka 2022 (CIFTIS) yanayoendelea hapa Beijing, mtangazaji wa moja kwa moja wa Sri Lanka anatambulisha biskuti na chai nyeusi kutoka Sri Lanka kwa wateja kote nchini China kwa kutumia simu ya mkononi.
Kwa mibofyo michache ya kidole, wateja wanaweza kununua wanasesere wa alpaca kutoka Peru, sabuni kutoka Syria, mchele na maharagwe ya kahawa kutoka Laos, na bidhaa nyingine kutoka nchi na maeneo yanayohusika na ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, huku bidhaa zikiwasilishwa moja kwa moja kwenye milango ya nyumba zao.
Kuongezeka kwa huduma kama hizo rahisi kunaweza kuhusishwa na mafanikio ya mtandao wa intaneti na biashara ya kidijitali. Katika maonyesho ya CIFTIS mwaka huu, wataalam wanasema kwamba teknolojia ya kidijitali imekuwa injini mpya ya ukuaji wa uchumi kwa nchi zilizoshiriki kwenye ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.
"Janga la UVIKO-19 limesababisha usumbufu ambao haujawahi kushuhudiwa," anasema Zhang Xiangchen, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani. "Hata hivyo, pia imekuwa kichocheo cha biashara duniani kote kuharakisha kwa kiasi kikubwa ugavi wa huduma kupitia mitandao ya kidijitali."
Kwa mujibu wa Zhang, uboreshaji wa kidijitali unaharakisha mzunguko mpya wa uvumbuzi katika huduma, ambao unatoa fursa kubwa za ukuaji wa uchumi. "Biashara ya kimataifa inaundwa mara kwa mara na kubadilishwa na uvumbuzi wa kiteknolojia."
Ripoti yenye kichwa cha "Biashara ya Kidijitali: Maendeleo na Ushirikiano," ambayo ilitolewa kwenye maonyesho ya CIFTIS, inaonyesha kuwa biashara ya kimataifa ya huduma za kidijitali ilizidi dola trilioni 3.8 za Marekani Mwaka 2021, ikiwa ni asilimia 63.6 ya jumla ya biashara ya huduma.
Biashara ya kidijitali ya China inaendelea kukua kwa kasi, huku jumla ya uagizaji na mauzo ya nje ya huduma za kidijitali ya China yakikua kwa asilimia 22.3 mwaka hadi mwaka Mwaka 2021 na kufikia dola za kimarekani bilioni 359.69.
"Njia ya hariri ya kidijitali ina nafasi kubwa katika ushirikiano wa hali ya juu wa ujenzi wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'," anasema Wang Xiaohong, Naibu Mkuu wa Idara ya Habari ya Kituo cha Mabadilishano ya Kiuchumi cha Kimataifa cha China.
"Teknolojia ya habari ya programu ya China, setilati ya mfumo wa urambazaji ya BeiDou, teknolojia ya blockchain na bidhaa na huduma nyingi za kidijitali, kama vile michezo ya kwenye kompyuta, uhuishaji, filamu na televisheni, zote zimetumika sana miongoni mwa nchi za‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ ," Wang anasema.
Kwenye Maonyesho ya CIFTIS Mwaka 2022, ambayo yalianza Jumatano, wiki iliyopita baadhi ya makampuni ya biashara kutoka nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” pia yalionyesha matumaini yao ya kufanya ushirikiano zaidi wa biashara ya kidijitali na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma