China yaboresha sekta ya viwanda ili kuleta uhakika wa uchumi wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 06, 2022

Mikono ya roboti ikikusanya injini kwenye karakana ya Kampuni ya Weichai Power katika Mji wa Weifang, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Aprili 22, 2021. (Xinhua/Guo Xulei)

JINAN - Katika kituo cha utengenezaji bidhaa kwa kutumia akili bandia cha Goertek katika Mji wa Weifang, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, tani za sehemu za vifaa zinaundwa kuwa zana katika Uhalisia Pepe (VR) ili kuwasilishwa kwa nchi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Chang Gang, naibu mkuu wa masoko na mauzo wa Goertek Inc., kiwanda hicho ni moja ya watengenezaji wachache wa zana za VR duniani kufikia kiwango cha uzalishaji cha seti milioni 1. Pia ni moja ya wazalishaji wakubwa wa earphone vichwa vya sauti vya kati na vya juu vya VR.

Kampuni ya Goertek ni kituo cha utengenezaji wa bidhaa wa hali juu cha China. Katika Maonyesho ya Mkutano wa Dunia wa Uzalishaji Bidhaa wa Hali ya Juu Mwaka 2022, ambao ulifungwa Ijumaa huko Jinan, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shandong, makampuni ya biashara na wataalam walikusanyika ili kujadili masuala ya mipaka ya maendeleo ya juu ya viwanda duniani.

Wataalamu walisema, China ikiwa ni mtengenezaji, mkuzaji thabiti na mboreshaji mkuu wa sekta ya utengenezaji bidhaa wa hali ya juu, inaleta uhakika kwa uchumi wa Dunia.

Takwimu za Wizara ya Viwanda na Tehama ya China zinaonyesha kuwa thamani ya ongezeko la sekta ya viwanda nchini China iliongezeka kutoka yuan trilioni 16.98 (kama dola trilioni 2.46 za Kimarekani) Mwaka 2012 hadi yuan trilioni 31.4 Mwaka 2021.

Ili kukuza mageuzi ya sekta ya viwanda, China imejenga mfumo wa kisasa wa viwanda unaoongozwa na sekta ya viwanda vya hali ya juu, na kukuza sekta ya viwanda ili kuendana na mnyororo wa thamani ulio wa kati na wa juu.

Kwa kuchukua tasnia ya injini zinazotumia dizeli ya China kama mfano, ufanisi wa joto wa injini za dizeli uliofanywa na Kampuni ya Weichai Holding sasa umezidi asilimia 51. Ikilinganishwa na bidhaa za msingi kwenye soko, matumizi ya kila mwaka ya mafuta na utoaji wa kaboni kwa aina hii ya injini umepunguzwa kwa asilimia 10.

Ban Ki-moon, katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, kupitia video fupi kwenye mkutano huo, alisema sekta ya viwanda ni nguzo ya maendeleo endelevu ya China na ukuaji wa uchumi wake. Alisema sekta hiyo imechangia kufikiwa kwa malengo ya Milenia ya Maendeleo Endelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.

Uelewa wa pamoja katika mkutano huo ulikuwa kwamba utandawazi wa uchumi wa dunia ni mwelekeo usioweza kubadilishwa, na uwazi na ushirikiano ni njia za kuendeleza sekta ya viwanda vya hali ya juu.

Kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda na Tehama, China itaendelea kutekeleza sera ya ufunguaji mlango wa hali ya juu wa sekta ya viwanda na kuboresha mazingira ya biashara. Wakati huo huo, China itahimiza makampuni ya ndani kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kuunganishwa katika mnyororo wa kimataifa wa viwanda, na kusaidia kukuza uchumi duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha