Shirika la OPEC+ latangaza kupunguza utoaji wa mafuta kwa kiasi kidogo Oktoba kutokana na bei kushuka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2022

Picha iliyopigwa tarehe 5, Septemba, 2022 ikionesha makao makuu ya Shirika la Nchi za kuuza mafuta kwa nchi za nje (OPEC) yaliyoko Vienna, Austria. (Xinhua/Wang Zhou)

Shirika la nchi za kuuza mafuta kwa nchi za nje (OPEC) na nchi wanachama wake, yaani shirika la OPEC+ Jumatatu wiki hii lilitangaza kupunguza utoaji wa mafuta kwa kiasi kidogo Mwezi Oktoba, ili kupandisha bei ya mafuta iliyoshuka kutokana na wasiwasi juu ya kudorora kwa uchumi.

Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa 32 wa mawaziri wa nchi za OPEC na zisizo za OPEC ilisema, shirika hilo limeamua kuwa, mwezi Oktoba litapunguza utoaji wa mafuta wa siku kwa mapipa 100,000 kutoka kwenye kiwango cha Mwezi Septemba.

Hii ni mara ya kwanza kwa shirika hilo kupunguza utoaji wa mafuta tokea mwaka mmoja uliopita. Kuanzia mwezi Agosti mwaka 2021, shirika hilo lilikuwa limeondoa hatua kwa hatua hali ya upunguzaji mkubwa wa utoaji wa mafuta iliyotokea katika kipindi kibaya zaidi cha maambukizi ya UVIKO-19.

Picha iliyopigwa tarehe 5, Septemba, 2022 ikionesha makao makuu ya Shirika la Nchi za kuuza mafuta kwa nchi za nje (OPEC) yaliyoko Vienna, Austria. (Xinhua/Wang Zhou)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha