“Wiki ya Utalii na Utamaduni wa China kwa Ng'ambo” ya Mwaka 2022 yaanzishwa Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 08, 2022

Hafla ya kuanzishwa kwa “Wiki ya Utalii na Utamaduni wa China kwa Ng'ambo” ya Mwaka 2022 ilifanyika Septemba 6, hapa Beijing. Waziri wa Utamaduni na Utalii Hu Heping alishiriki kwenye hafla hiyo na kutoa hotuba. Mkuu wa gazeti la People's Daily, Tuo Zhen, mjumbe wa kamati ya wahariri wa People's Daily ambaye pia ni mhariri mkuu wa toleo la ng'ambo, Chen Zhi, walishiriki kwenye hafla hiyo.

Hafla ya kuanzishwa kwa “Wiki ya Utalii na Utamaduni wa China kwa Ng'ambo” ya Mwaka 2022 ilifanyika Beijing. (Mpiga picha: Yukai/People's Daily Online)

Waziri wa Utamaduni na Utalii Hu Heping, Mkuu wa Gazeti la People's Daily, Tuo Zhen na mjumbe wa Kamati ya wahariri wa Gazeti la People's Daily ambaye pia ni mhariri mkuu wa toleo la ng'ambo, Chen Zhi walishiriki kwenye hafla hiyo. (Mpiga picha: Xu Zheng/People's Daily Online)

Shughuli hizo za “Wiki ya Utalii na Utamaduni wa China kwa Ng'ambo”iliandaaliwa na Kituo cha Utamaduni wa China kwa ng’ambo, Ofisi za utalii za nje ya nchi na gazeti la mtandaoni la People's Daily, ikiwa na mada tano ambazo ni " Endeleza shughuli za Urithi wa Utamaduni Usioshikika kwa kuondoa umaskini", " Kustawisha Vijiji ", "Ujenzi wa Miji", "Utamaduni wa Mto Manjano" na "Utalii wa Kitamaduni wa Njia ya Hariri", maonesho ya mada maalum, maonesho ya video na semina, yote hayo yatafanyika kwa ajili ya watazamaji wa ndani na nje ya nchi kwenye ukumbi na kwa njia ya video.

Hu Heping alitoa hotuba akisema kuwa shughuli hizo zitaonesha ipasavyo mafanikio makubwa yaliyopatikana katika ujenzi wa ujamaa wenye umaalum wa China katika zama mpya kwa kupitia kusimulia hadithi kuhusu kuhifadhi na kurithi utamaduni bora wa jadi wa China, utamaduni na utalii kusaidia kuondokana na umaskini na kustawisha vijiji. Wizara ya Utamaduni na Utalii itachukulia shughuli hizo kama fursa ya kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na nchi mbalimbali duniani katika utamaduni na utalii.

Katika hafla ya uzinduzi, matawi 9 ya ukumbi wa mkutano ya Guiyang Mkoani Guizhou, Ganzhou Mkoani Jiangxi, Hangzhou Mkoani Zhejiang, Zhengzhou Mkoani Henan, Xi'an Mkoani Shaanxi, Ofisi ya Utalii ya China iliyoko huko Frankfurt, Kituo cha Utamaduni cha China kilichopo Tokyo na Matawi ya gazeti la mtandaoni la People's Daily nchini Japan na Korea ziliunganishwa na ukumbi mkuu wa mkutano wa Beijing kwa njia ya mtandao wa intaneti. Washiriki kutoka Uingereza, Ujerumani, Italia, Ufaransa, Australia, Thailand, Mexico, Misri, Nigeria na nchi nyingine walipongeza kuanzishwa kwa "Wiki ya Utalii na Utamaduni wa China kwa Ng'ambo" ya Mwaka 2022 kwa njia ya video. Katika halfa hiyo, jukwaa la kujifunza lugha nyingi la "Masomo ya Utalii ya China" lilitangazwa kwa watu duniani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha