Biashara ya nje ya China yadumisha ukuaji huku kufufuka kwa uchumi kukiimarka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 08, 2022

Picha iliyopigwa Tarehe 9 Juni 2022 kutoka angani ikionyesha kituo cha kontena katika Bandari ya Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Picha na Yu Fangping/Xinhua)

BEIJING - Biashara ya nje ya China ilidumisha kasi ya ukuaji katika miezi minane ya kwanza ya mwaka, ikiwa ni ishara chanya ya kuimarika kwa uchumi, huku serikali ikiendelea kuweka hatua za kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta utulivu wa biashara ya nje.

Takwimu rasmi za Serikali ya China Jumatano zilionesha kuwa, katika miezi minane ya kwanza ya mwaka huu, biashara ya nje ya China ya bidhaa iliongezeka kwa asilimia 10.1 kuliko ile ya kipindi kama hiki cha mwaka jana, na kufikia yuan trilioni 27.3 (kama dola trilioni 3.95 za Kimarekani) katika miezi minane ya kwanza.

Kwa masharti ya dola ya Marekani, jumla ya biashara ya nje ilikuwa dola za Marekani trilioni 4.19 katika miezi minane, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.5 kuliko mwaka jana.

Idara Kuu ya Forodha ya China (GAC) imesema, mauzo ya nje yalipanda kwa asilimia 14.2 na kufikia yuan trilioni 15.48. Uagizaji bidhaa uliongezeka kwa asilimia 5.2 kutoka mwaka mmoja uliopita hadi kufikia yuan trilioni 11.82, na kusababisha ziada ya biashara yenye thamani ya yuan trilioni 3.66.

Mwezi Agosti pekee, kiwango cha biashara ya nje nchini China kilipanda kwa asilimia 8.6 na kufikia yuan trilioni 3.71, mauzo ya nje na uagizaji wa bidhaa kutoka nje yameongezeka kwa asilimia 11.8 na asilimia 4.6 kuliko mwaka jana.

Kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu, biashara ya China na washirika wenzi wake wakuu watatu wa kibiashara -- Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN), Umoja wa Ulaya, na Marekani -- iliongezeka kwa asilimia 14, asilimia 9.5 na asilimia 10.1.

Katika kipindi hicho, biashara ya China na nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja ilipanda kwa asilimia 20.2 na kufikia yuan trilioni 8.77.

Uuzaji nje wa bidhaa za mitambo na kielektroniki uliongezeka kwa asilimia 9.8 hadi kufikia jumla ya asilimia 56.5, na mauzo ya nje ya bidhaa zinazohitaji nguvu kazi kubwa yaliongezeka kwa asilimia 14.1 kuliko mwaka uliopita.

"Ukuaji wa kasi wa biashara ya nje ya China katika miezi minane ya kwanza umekuja wakati ambapo China inaendelea kutekeleza sera za kuleta utulivu wa biashara ya nje na kuratibu udhibiti wa janga la UVIKO na maendeleo ya kiuchumi na kijamii," amesema Li Kuiwen, msemaji wa GAC.

Pamoja na kutunga mlolongo wa sera za kuleta utulivu wa uchumi Mwezi Mei, China ilianzisha sera 19 za ziada za ufuatiliaji ili kuleta harambee kubwa, kwa mujibu wa uamuzi uliotolewa katika mkutano mkuu wa Baraza la Serikali la China Mwezi Agosti.

Jumatatu wiki hii Waziri Msaidizi wa Biashara wa China Li Fei alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, wizara hiyo iliweka mikakati ya kukuza mifumo mipya ya biashara kama vile biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka na biashara ya ununuzi wa soko ili kuleta utulivu wa biashara ya nje. Wizara hiyo pia itatoa msaada zaidi kwa uuzaji nje wa magari yanayotumia nishati mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha