Rais wa Burundi afanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 09, 2022

BUJUMBURA - Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri huku sura tano mpya zikiingia.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa Alhamisi jioni kwenye redio na televisheni ya Serikali ya Burundi na msemaji wa rais, imesema kuwa, mawaziri wapya watano wataingia kwenye baraza la mawaziri linaloundwa na mawaziri 15.

Sanctus Niragira, Chansela wa Chuo Kikuu cha Burundi, anachukua nafasi ya Deo Guide Rurema kuwa waziri wa mazingira, kilimo na mifugo.

Dieudonne Dukundane anachukua nafasi ya Deogratias Nsanganiyumwami kuwa waziri wa miundombinu, vifaa na makazi ya jamii.

Martin Niteretse, katibu mkuu katika wizara ya mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama wa umma, anachukua nafasi ya Gervais Ndirakobuca kuwa waziri mpya wa wizara hiyo. Ndirakobuca aliteuliwa na rais Jumatano wiki hii kuwa waziri mkuu mpya kuchukua nafasi ya Alain Guillaume Bunyoni, ambaye alishutumiwa kwa kuhujumu shughuli za serikali.

Audace Niyonzima anachukua nafasi ya Domitien Ndihokubwayo kuwa waziri mpya wa fedha, bajeti na mipango ya uchumi, na Deogratias Rusengwamihigo anachukua nafasi ya Thaddee Ndikumana kuwa waziri wa utumishi wa umma, kazi na ajira.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha