

Lugha Nyingine
Huduma za treni za mizigo kati ya China na Ulaya zashuhudia ukuaji imara Mwezi Agosti
Treni inayotoa huduma za kubeba mizigo kati ya China na Ulaya ikiwasili kwenye Bandari ya Kimataifa ya Xi'an huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi Kaskazini-Magharibi mwa China, Agosti 31, 2022. (Xinhua/Li Yibo)
BEIJING - Idadi ya huduma za treni ya mizigo kati ya China na Ulaya iliongezeka kwa asilimia 18 mwezi uliopita kuliko mwaka jana, na kufikia rekodi ya juu ya safari 1,585, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli la China.
Habari zinasema, takriban mabehewa 154,000 ya mizigo yenye ukubwa wa futi 20 yalisafirisha bidhaa kupitia treni za mizigo Mwezi Agosti, ikiwa ni ongezeko la asilimia 19 kutoka mwaka mmoja uliopita.
Katika miezi minane ya kwanza mwaka huu, idadi ya safari za treni za mizigo kati ya China na Ulaya iliongezeka kwa asilimia 5 na kufikia 10,575. Treni hizo zilisafirisha jumla ya bidhaa za TEU milioni 1.02, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6 kutoka mwaka mmoja uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma