Mtu mmoja asimamia bustani ya matunda ya hekta 66.7 kwa kutegemea teknolojia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 14, 2022

Kituo kimoja kikubwa cha Upandaji wa matunda ya pitaya katika Mji wa Nanning. (Picha na Idara ya Ustawishaji wa Vijiji ya Nanning)

Mji wa Nanning wa Mkoa wa Guangxi una kituo kikubwa zaidi cha upandaji wa matunda ya pitaya duniani, ambapo upandaji wake unategemea teknolojia ya hali ya juu na mbinu za usimamizi za ndani na nje ya China.

Kampuni ya Kilimo ya Jianian ya Guangxi inatumia maarifa yake ya usimamizi wa viwanda na mbinu za uendeshaji, usimamizi na uuzaji zilizopatikana katika uzoefu wa miaka mingi kwenye uzalishaji wa viwanda, ikiongoza maendeleo ya uzalishaji wa kilimo, imepata ufanisi wa uzalisha kwa kiasi kikubwa.

Liao Xiangsong, msimamizi mkuu wa ufundi wa Kampuni ya Kilimo ya Jianian, alisema kuwa kwa kutegemea msaada wa teknolojia ya kisasa ya usimamizi wa uzalishaji, mume na mke wake wawili tu wanaweza kusimamia kirahisi kazi kwenye mashamba ya zaidi ya hekta 2.22. “msimamizi mmoja anaweza kukamilisha kazi zote za uratibu kwenye mashamba ya hekta 66.7.”

Hivi sasa, matunda ya pitaya ya Nanning yanauzwa kote nchini China. Zaidi ya hayo, pamoja na shehena ya kwanza ya matunda ya pitaya kusafirishwa nchini Uholanzi Mwezi Januari, 2021, matunda ya pitaya ya Nanning pia yameanza kuingia kwenye soko la kimataifa na kwenda nje ya nchi hatua kwa hatua.

Muonekano wa hali ya jioni ya Kituo cha Upandaji wa matunda ya pitaya katika Mji wa Nanning. (Picha na Idara ya Kustawisha Vijiji ya Nanning)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha