Rais Xi Jinping akutana na rais Ukhnaa Khurelsukh wa Mongolia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 16, 2022

Rais Xi Jinping wa China akikutana na rais Ukhnaa Khurelsukh wa Mongolia kwenye Hoteli ya Wageni wa Taifa ya Samarkand, Uzbekistan mchana wa tarehe 15 kwa saa za Samarkand. (Xinhua/Cui Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China alikutana na rais Ukhnaa Khurelsukh wa Mongolia kwenye Hoteli ya Wageni wa Taifa ya Samarkand, Uzbekistan mchana wa tarehe 15 kwa saa za Samarkand.

Rais Xi alisema, uhusiano kati ya China na Mongolia unadumisha mwelekeo wa maendeleo mazuri, mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali vimepata matunda makubwa. Upande wa China unaweka uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwenye nafasi muhimu ya mambo ya diplomasia na nchi jirani, na ungependa kuhimiza urafiki wa jadi pamoja na upande wa Mongolia, kupanua ushirikiano wa kunufaishana, na kusukuma uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Mongolia kupanda ngazi ya juu zaidi.

Ukhnaa Khurelsukh alisema, urafiki wa jadi kati ya Mongolia na China unaimarika siku hadi siku, uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili ni mfano wa kuigwa wa uhusiano kati ya nchi na nchi. Upande wa Mongolia unasifu sana mchango muhimu uliotolewa na China katika kulinda amani na usalama wa dunia, na ungependa kuhimiza ushirikiano wa kivitendo na China katika sekta za uchumi na biashara, reli, na mazingira.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha