Utafiti wa kwanza wa China kwenye sayari Mars wapata matunda mbalimbali ya kisayansi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 19, 2022

Idara ya kitaifa ya Safari ya Anga ya Juu ya China (CNSA) Jumapili ya wiki iliyopita ilisema, utafiti wa kwanza wa China kwenye sayari ya Mars umepata matunda kemkem ya kisayansi.

Idara hiyo ilisema, hadi Alhamisi ya wiki iliyopita, chombo cha utafiti kwenye obiti cha “Tianwen 1” kimeendeshwa katika hali ya kawaida kwa siku zaidi ya 780, na kigari cha Mars “Zhurong” kimetembea kwa mita 1,921 kwenye ardhi ya sayari ya Mars.

Chombo cha utafiti kwenye obiti cha “Tianwen 1” na kigari chake cha kutembea kwenye Mars vimemaliza kazi za utafiti wa kisayansi zenye malengo, na vimepata tarakimu asilia za kisayansi za 1480G.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha