China na Russia zafanya mkutano kuhusu mfumo wa ushirikiano wa utekelezaji wa sheria na usalama

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 20, 2022

Guo Shengkun, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Siasa na Sheria ya Kamati Kuu ya CPC, akiwa pamoja na Nikolai Patrushev, Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia kwenye mkutano wa 7 wa mfumo wa ushirikiano wa utekelezaji wa sheria na usalama kati ya China na Russia uliofanyika Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China, Septemba 19, 2022. (Xinhua/Jiang Kehong)

FUZHOU - Guo Shengkun, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Jumatatu wiki hii ameongoza mkutano wa 7 wa mfumo wa ushirikiano wa utekelezaji wa sheria na usalama kati ya China na Russia pamoja na Nikolai Patrushev, Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, katika Mkoa wa Fujian Mashariki mwa China.

Guo, ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Siasa na Sheria ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amesema chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Russia wa uratibu wa zama mpya umedumisha maendeleo mazuri na ya utulivu.

Amesema, tangu kuanzishwa kwa mfumo wa utekelezaji wa sheria na usalama, China na Russia zimeshirikiana kwa karibu katika kulinda usalama wa kisiasa wa taifa, kupambana na ugaidi, udhibiti wa dawa za kulevya na kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka. Amesema, mfumo huo umepata matokeo mazuri na umechukua nafasi isiyoweza kubadilishwa katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo ya nchi hizo mbili.

Guo amesema China inapenda kushirikiana na Russia katika kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili wakati wa mkutano wa kilele wa SCO uliofanyika huko Samarkand, Uzbekistan.

“China itatekeleza kikamilifu jukumu la mfumo wa utekelezaji wa sheria na usalama ili kukabiliana na hatari na changamoto mbalimbali za kiusalama.” Amesema Guo.

Kwa upande wake, Patrushev amesema Russia iko tayari kwa mazungumzo ya karibu na China katika ngazi zote ili kuweka mazingira mazuri ya usalama kwa ajili ya maendeleo mazuri ya ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha