Tetemeko la ardhi latokea nchini Mexico

(CRI Online) Septemba 20, 2022

Idara ya Taifa ya Tetemoko la Ardhi nchini Mexico imesema, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.7 kwenye kipimo cha richter limetokea katika jimbo la Michoacan jana na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Huduma ya Tahadhari dhidi Tsunami ya nchini Marekani imesema, huenda tsunami kubwa inaweza kutokea kwenye ufukwe uliopo ndani ya kilomita 300 kutoka kwenye kitovu cha tetemeko hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha