Maonesho ya China-Eurasia yaweka rekodi mpya ya kufikia Biashara yenye thamani ya Yuan bilioni 960

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 21, 2022

Mtembeleaji akitazama roboti ya kufanya upasuaji kwenye Maonesho ya saba ya China-Eurasia yaliyofanyika Urumqi, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiensha wa Xinjiang Uygur wa Kaskazini Magharibi mwa China tarehe 20, Septemba. (Xinhua/Ding Lei)

Thamani ya jumla ya biashara zilizofikiwa imeweka rekodi mpya ya kihistoria kwenye Maonesho ya saba ya China-Eurasia yaliyofanyika kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 22, Septemba huko Urumqi, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur wa Kaskazini Magharibi mwa China, walisema waandalizi wa maonesho hayo Jumanne ya wiki hii.

Hadi hivi sasa, thamani ya jumla ya biashara zilizofikiwa imezidi Yuan bilioni 960 (takriban Dola za Marekani bilioni 138.19), ikiwa ni mara tatu ya ile ya maonesho yaliyopita ya mwaka 2018.

Maonesho ya mwaka huu yalifanyika kwenye mtandao wa intaneti na pia kwenye jumba la maonesho. Yaliweka mkazo katika miradi yenye mustakabali mzuri, kiwango cha juu cha kiteknolojia, na mahitaji makubwa ya uwekezaji. Yaliandaa shughuli za kuhimiza uwekezaji na biashara, na kujenga jukwaa kwa hamasa kwa ajili ya biashara ya ngazi ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha