Uchumi wa Afrika wakabiliwa na tishio la msukosuko wa hali ya hewa na mashaka juu ya kanuni

(CRI Online) Septemba 21, 2022

Wataalam wa Afrika wamesema, msukosuko wa hali ya hewa na wasiwasi wa kisiasa na kanuni vinatishia ukuaji endelevu wa uchumi wa Afrika.

Wakizungumza katika mkutano wa kutolewa kwa ripoti ya mwaka 2022 ya Viashiria vya Hatari na Faida za Uchumi wa Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao, wataalam hao wamesema bara hilo linapaswa kukabiliana na matishio yanayoibuka ya mapigano, msukosuko wa hali ya hewa, na wasiwasi wa kisiasa na kanuni ili kudumisha ukuaji wa uchumi.

Ripoti hiyo imesema, ukuaji wa baadaye wa Afrika utategemea zaidi katika matumizi ya nishati mpya, uwekezaji katika mfumo wa chakula unaovumilia mabadiliko ya hali ya hewa, kuongeza kasi ya maingiliano, na usimamizi mzuri wa fedha za umma.

Mchambuzi mwandamizi katika Kituo cha Kudhibiti Hatari cha Afrika Magharibi, Patricia Rodrigues amesema, nia ya Afrika ya ufufuaji wa uchumi iko hatarini kutokana na vurugu zinazohusiana na janga la COVID-19, vita kati ya Ukraine na Russia, na ukame unaoendelea.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha