Rais Xi Jinping asisitiza kuanzisha hali mpya ya mageuzi kwa kuimarisha jeshi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2022

Kongamano la mageuzi ya mambo ya ulinzi na jeshi lilifanyika Beijing tarehe 21, Septemba. Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye pia ni rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi Xi Jinping alitoa agizo muhimu.

Alisisitiza kuwa, tangu mkutano mkuu wa 18 wa CPC ulipofanyika, Kamati Kuu ya CPC na Kamati Kuu ya Kijeshi zikiwa na nia thabiti na nguvu kubwa kuliko hapo kabla, zimetekeleza kikamilifu mkakati wa mageuzi kwa kuimarisha jeshi, kuondoa vizuizi vya kimfumo, migongano ya muundo na matatizo ya kisera, ambavyo vinazuia kwa muda mrefu ujenzi wa mambo ya ulinzi na jeshi, na kuendeleza kwa kina mageuzi ya mambo ya ulinzi na jeshi, ili kupata mafanikio ya kihistoria.

Xi alitaka kufanya majumsho kwa makini na kutumia maarifa ya kufanikisha mageuzi, kuelewa hali mpya na matakwa mapya ya majukumu , na kuweka mkazo kwenye matayarisho ya kupambana.

Xi alidhihirisha kuwa, ni muhimu kufanya uvumbuzi na kuimarisha kupanga mageuzi yajayo, ili kutoa msukumo mkubwa kwa ajili ya kutimiza malengo ya miaka 100 ya kuanzishwa kwa jeshi la China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha