Kenya yatangaza utafiti wa utangulizi kuhusu ugonjwa wa Alzheimer

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2022

(Picha inatoka CFP.)

Mtafiti wa matibabu wa Kenya Jumatano ya wiki hii alisema kuwa, nchi hiyo imetangaza utafiti kamili wa kwanza wa kihistoria ili kuchora ramani ya kuenea kwa ugonjwa wa Alzheimer na ugonjwa wa shida ya akili.

Mtafiti wa Mfuko wa utafiti na mafunzo ya afya ya kisaikolojia wa Afrika (AMHRTF) Christine Musyimi alisema, watafanya uchunguzi wa shida ya akili miongoni mwa watu 2400 wenye umri wa zaidi ya miaka 60 kutoka Wilaya ya Makueni, Mashariki mwa Kenya, ili kukadiria mzigo unaoletwa na ugonjwa huo.

“Hadi hivi sasa hatuna takwimu zilizotolewa na serikali kuhusu ugonjwa wa Alzheimer na ugonjwa wa shida ya akili, na idadi kubwa ya sampuli zitatutolea takwimu ambazo zinaweza kutumika kwa kukadiria idadi ya wagonjwa wa nchi nzima. Uchunguzi utafanywa na wahudumu wanaojitolea wa maeneo ya makazi waliofundishwa vizuri,” alisema Musyimi.

Alitoa hotuba Jumatano ya wiki hii kwenye shughuli ya kukumbuka siku ya Alzheimer ya kimataifa iliyofanyika Nairobi, Kenya, ambapo Shirika la kimataifa la ugonjwa wa Alzheimer (ADI) lilitoa ripoti kuhusu ugonjwa wa Alzheimer duniani katika mwaka 2022.

AMHRTE ni shirika lisilo la kiserikali, nalo linatekeleza mradi huo chini ya msaada wa kifedha wa shirika la ushirikiano wa ugonjwa wa Alzheimer la Davos (DAC). 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha