Kituo cha Kompyuta za Akili Bandia cha China-ASEAN kitatangazwa Nanning, Guangxi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2022

Muonekano wa mkutano na waandishi wa habari wa Mkutano wa 3 kuhusu Akili Bandia wa China (Guangxi)-ASEAN.(Mpiga picha: Wang Gongxiao/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Hivi karibuni, Ofisi ya Habari ya Serikali ya Mkoa unaojiendesha wa Wazhuang wa Guangxi ilifanya mkutano na waandishi wa habari wa Mkutano wa 3 kuhusu Akili Bandia wa China (Guangxi)-ASEAN. Habari zilizotolewa kwenye mkutano huo zikisema, Kituo cha Kompyuta za Akili Bandia cha China-ASEAN kilichojengwa kwa uwekezaji wa Mji wa Nanning kitatangazwa kwenye Mkutano wa 3 kuhusu Akili Bandia wa China (Guangxi)-ASEAN utakaofanyika Septemba 23.

Habari zilisema kuwa, Kituo cha Kompyuta za Akili Bandia cha China-ASEAN kinatumia teknolojia ya akili bandia ya Ascend ambayo China inaweza kuidhibiti kikamilifu na kujenga jukwaa la msingi la akili bandia la China.

Kituo cha Kompyuta za Akili Bandia cha China-ASEAN kikiwa mradi muhimu wa kituo cha Tehama cha China-ASEAN kitajenga miundombinu ya aina mpya mjini Guangxi, ambayo inaweza kufanya kazi katika kusini-magharibi na kati-kusini, na kuelekea ASEAN. Katika nyanja za teknolojia muhimu za nguvu ya kompyuta, njia za mahesabu na data, itaimarisha ushirikiano katika kufanya uvumbuzi, na kuweka mkazo katika maunganisho na matumizi, ili kutoa nguvu ya tegemezi kwa ajili ya mawasiliano na ushirikiano kati ya China na nchi za ASEAN na maeneo yao katika nyanja ya uchumi wa kidijitali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha