Putin asema viwanda vya ulinzi vya Russia lazima vizalishe bidhaa za Russia kwa asilimia mia moja badala ya zile zilizoagizwa kutoka nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2022

Rais wa Russia Vladimir Putin alisema tarehe 20 kwamba viwanda vya ulinzi vya Russia lazima vizalishe bidhaa za Russia kwa asilimia mia moja badala ya zile zilizoagizwa kutoka nchi za nje, ambapo vinatakiwa kuongeza uwezo wa uzalishaji na kupunguza muda wa uzalishaji katika hali ya kutoathiri ubora wa bidhaa.

Putin alisema hayo siku hiyo alipokutana na wakuu wa makampuni ya viwanda vya ulinzi vya Russia. Alisema, Russia ina haja ya kuongeza uwezo wa uzalishaji wa viwanda vya ulinzi, na kuvifanyia mageuzi ili viwe vya kisasa katika wakati wa lazima. Pia alisema, mwaka huu utoaji wa silaha na zana kwa majeshi ya Russia utaongezeka, tena fedha zitatolewa kwa ajili ya kununua na kutengeneza silaha na zana za kijeshi.

Putin alisema, silaha na zana zilizotengenezwa na Russia zimeonyesha ufanisi wa juu katika operesheni maalum ya kijeshi na zinaweza kukabiliana na silaha za Magharibi. Ameongeza kuwa, silaha za kijeshi zilizotengenezwa na Russia zinachukua nafasi thabiti katika soko la silaha duniani, na katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, Russia ilitoa silaha zenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 6 kwa washirika wake wa ng'ambo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha