Watu wawili wafariki katika tetemeko la ardhi nchini Mexico

(CRI Online) Septemba 22, 2022

Wizara ya ulinzi wa raia ya  Mexico imesema, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.7 kwenye kipimo cha Richter lililotokea katika jimbo la Michoacán limesababisha vifo vya watu wawili na wengine 10 kujeruhiwa.

Gavana wa jimbo hilo Bw. Alfredo Ramirez Bedoría amesema, zaidi ya nyumba 3,000 na hospitali 20 ziliharibiwa katika tetemeko la ardhi, ambalo pia lilisababisha maporomoko ya ardhi yaliyoziba baadhi ya barabara. Amesema kazi ya kusafisha barabara hizo bado inaendelea.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha