Ukame mkali kuwaathiri watu milioni 36.1 katika Pembe ya Afrika

(CRI Online) Septemba 23, 2022

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeonya kuwa, takriban watu milioni 36.1 kwenye Pembe ya Afrika, wakiwemo milioni 24.1 nchini Ethiopia, milioni 7.8 nchini Somalia, na milioni 4.2 nchini Kenya, wataathiriwa na ukame mkali mwezi Oktoba.

OCHA imesema idadi hiyo imeongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwezi Julai wakati ambapo watu milioni 194 waliathiriwa na ukame, na mashirika ya utoaji wa misaada yamechukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo ya dharura.

Pia imesema nchi za Pembe ya Afrika zinakabiliwa na tishio la njaa, huku utabiri wa hali ya hewa ukionesha kuwa, ukosefu wa mvua utaendelea katika msimu wa mvua wa Oktoba-Desemba katika baadhi ya sehemu za Ethiopia, Kenya, na Somalia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha