Rais wa Somalia aahidi nchi hiyo iko tayari kupambana na baa la njaa na ugaidi

(CRI Online) Septemba 23, 2022

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ametoa wito kwa wenzi wa kimataifa kusaidia juhudi za nchi hiyo kuepuka baa la njaa na kushinda ugaidi.

Akizungumza katika Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa, rais Mohamud amesema, licha ya juhudi za miongo miwili za kudhibiti mapigano, ukame, njaa na kudorora kwa maendeleo ili kufikia zama mpya za utulivu, maendeleo na ustawi, bado Somalia inakabiliwa na hali ngumu inayohusiana na msukosuko wa hali ya hewa unaoendelea duniani kwa sasa.

Ameitaja msukosuko huo kuwa ni pamoja na ukame unaoendelea kukumba nchi hiyo, ambao unatishia maisha ya jamii zilizo hatarini zaidi nchini humo.

Ametoa wito kwa wenzi wote wa nchi hiyo kufanya kila linalowezekana kuisaidia nchi hiyo kuepukana na tishio la ukame, ambalo linaikabili kanda ya Pembe ya Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha