Jeshi la Nigeria lawaua wapiganaji wenye msimamo mkali

(CRI Online) Septemba 23, 2022

Jeshi la Nigeria limesema limefyatua risasi na kuwaua wapiganaji 36 wenye msimamo mkali na kuwaokoa raia 130 waliotekwa nyara katika operesheni ya kijeshi iliyofanyika kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wiki mbili zilizopita.

Msemaji wa jeshi la Nigeria Bw. Moussa Danmadami amesema, operesheni hiyo inalenga kupambana na makundi ya Boko Haram na IS ambayo yamekaa kwa muda mrefu kaskazini mashariki mwa Nigeria. Ameongeza kuwa, wapiganaji 46 na watu 12 wanaoshukiwa kutoa huduma kwa wapiganaji hao walikamatwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha