Rais wa China azitaka serikali za ngazi zote nchini humu kuhimiza ustawi wa vijiji

(CRI Online) Septemba 23, 2022

Mkulima akiendesha mashine kuvuna mpunga huko Changchun, Mkoa wa Jilin wa Kaskazini Mashariki mwa China Septemba 20, 2022. (Picha/Xinhua)

Rais wa China Xi Jinping ametoa pongezi na salamu kwa wanavijiji na wafanyakazi wanaoshughulikia sekta ya kilimo wakati Siku ya Tano ya Mavuno ya Wakulima nchini China ikikaribia.

Rais Xi amezitaka serikali za ngazi zote kutekeleza kihalisi sera zilizotungwa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kilimo, wakulima na vijiji. Pia kuimarisha uhakikishaji wa usalama wa nafaka, kutuliza sekta ya kilimo, kupanua mafanikio ya kuondoa umaskini, na kuhimiza ustawi wa vijiji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha