Mapato ya usafirishaji ya Reli ya Ethiopia-Djibouti yaendelea kuongezeka kwa kasi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2022
Mapato ya usafirishaji ya Reli ya Ethiopia-Djibouti yaendelea kuongezeka kwa kasi
Septemba 19, dereva mmoja akifanya maandalizi ndani ya treni kabla ya kufunga safari.

Reli ya Ethiopia-Djibouti iliyojengwa na kuendeshwa kwa pamoja na Idara ya 11 ya Kampuni ya Reli ya China na Kampui ya Kundi la Ujenzi na Uhandisi la China, inaunganisha Ethiopia na Djibouti, ni reli ya kwanza ya kuvuka nchi inayotumia umeme barani Afrika, na urefu wake unafikia kilomita 752.7. Tangu kuzinduliwa rasmi kwa reli hiyo Mwaka 2018, huduma za usafirishaji wake zinaongezeka kuwa mengi, na mapato ya usafirishaji yanadumisha ongezeko la kasi. Mwaka 2021, kwenye reli hiyo kulikuwa na treni 449 za abiria na treni 1469 za mizigo, ambapo pia yalisafirishwa kwa makontena 77,357.

(Mpiga picha: Dong Jianghui/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha