Mtandao wa maeneo ya biashara huria ya China wachangia dhahiri thamani ya jumla ya biashara na nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2022

Picha iliyopigwa tarehe 13, Septemba, 2022 ikionesha meli inayotia nanga kwenye gati la makontena la Bandari ya Qinzhou ya Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Shu Jueting Alhamisi alisema, tangu China ilipojiunga na WTO mwaka 2001, China imekuwa ikipanua mtandao wake wa maeneo ya biashara huria.

Hadi hivi sasa, China imesaini mikataba 19 ya biashara huria na nchi na maeneo 26, wenzi wake wa ushirikiano wako katika sehemu mbalimbali za Asia, Oceania, Bara la Latin Amerika, Ulaya na Afrika.

Msemaji huyo alisema, thamani ya biashara kati ya China na wenzi wake wa biashara huria inachukua asilimia 35 hivi ya thamani ya jumla ya biashara ya China na nje.

Shu alisema, China itasaini mikataba mingi zaidi ya biashara huria na wenzi wake wenye nia ya ushirikiano, na kufanya juhudi za kuongeza ufanisi wa mikataba hiyo, ili kuleta manufaa mazuri na haraka kwa kampuni na watu wa nchi husika. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha