Mwakilishi wa China kwenye Baraza la Haki za Binadamu la UM ahimiza Marekani kuacha uingiliaji haramu wa kijeshi katika Syria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2022

Mwakilishi wa China Jiang Duan tarehe 22 kwenye Mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UM) alilaumu vikali uingiliaji haramu wa kijeshi wa Marekani dhidi ya Syria na vitendo vingine vyake vinavyodhuru haki za binadamu za kimsingi za watu wa Syria, na amehimiza Marekani kuacha mara vitendo hivyo.

Bw. Jiang Duan alisema, Marekani inafanya uingiaji wa kijeshi mara kwa mara dhidi ya Syria, ambao umesababisha vifo na majeruhi na kukimbia makazi kwa raia wengi, na kuleta hasara ya mali isiyohesabika.

Jiang Duan alisema, msukosuko wa Syria umeonesha kuwa, uingiliaji kutoka nje, uchochezi wa mapambano na uwekeaji wa vikwazo havisaidii kutatua matatizo. China siku zote inatetea kutatua matatizo kwa njia ya kisiasa. Ameihimiza Marekani kuacha kukaa kiharamu nchini Syria, kuacha vitendo vyake haramu vya kijeshi katika Syria, kusimamisha vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Syria, kuacha kuiba mafuta na chakula kutoka Syria, na kuwarudishia watu wa Syria haki za binadamu za kweli, mali, uhuru na heshima.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha