Wajumbe wote watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC wamechaguliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2022

Taarifa rasmi iliyotolewa Jumapili iliyopita ikisema kuwa, wajumbe 2,296 waliochaguliwa watahudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Wajumbe hao walichaguliwa kwa kufuata njia iliyowekwa na Kamati Kuu ya Chama, na kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama na Kamati Kuu ya Chama chini ya mwongozo wa fikra ya Xi Jinping kuhusu ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya.

Mchakato huo wa kuwachagua wajumbe ulifuata asili na nia ya Chama, kushikilia na kuimarisha uongozi wa Chama kwa pande zote, na kuonesha kikamilifu demokrasia ya ndani ya chama.

Wajumbe hao wanaundwa na wanachama bora wa CPC ambao wana sifa bora ya kifikra na kisiasa, ni wenye mienendo mizuri ya kazi na maisha, wenye uwezo wa kujadili masuala, na waliopata mafanikio dhahiri katika kazi zao.

Uundaji na utapakaaji wa wajumbe hao ni wa kufaa, ambao unafuata matakwa ya Kamati Kuu ya Chama, na unawakilisha watu wa sehemu mbalimbali nchini China.

Miongoni mwa wajumbe hao kuna wanachama ambao ni maofisa viongozi, wanaofanya kazi kwenye mstari wa mbele wa uzalishaji, pia kuna idadi inayofaa ya wanachama wanawake, wanachama wa makabila madogo madogo, pamoja na wajumbe wa sekta mbalimbali za uchumi, sayansi na teknolojia, ulinzi wa nchi , siasa na sheria, elimu, uenezi, utamaduni, afya, michezo na usimamizi wa jamii.

Wajumbe watakaohudhuria kwenye mkutano mkuu wa 20 wa Chama watathibitishwa tena baadaye na kamati ya ukaguzi. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha