Ofisi husika yatoa habari zaidi kuhusu uchaguzi wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 27, 2022

Picha iliyopigwa Mei 22, 2020 ikionyesha bendera kwenye Uwanja wa Tian'anmen na sehemu ya juu ya Jumba la mikutano ya umma la Beijing. (Picha: Xinhua)

Ofisi husika ya China ilitoa habari zaidi kuhusu kuwachagua wajumbe watakaohudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) baada ya kutangaza Jumapili ya wiki iliyopita kuwa wajumbe wote 2,296 wameshachaguliwa.

Ofisa husika wa ofisi ya oganezeshi ya Kamati Kuu ya Chama alisema, kazi zote za uchaguzi zilizoanzia Novemba, 2021 hadi Julai, 2022 zimekamilika, na wajumbe wote ni wanachama wenye sifa bora wa CPC.

Wajumbe hao wanawakilisha watu wa sehemu mbalimbali. Kwa jumla wajumbe 771 wanatoka mstari wa mbele wa uzalishaji wakichukua asilimia 33.6 ya idadi ya jumla ya wajumbe. Miongoni mwa wajumbe hao wapo wafanyakazi au wakulima wanaofanya kazi mijini 192, wakulima 85, na mafundi wa kazi maalum 266.

Ofisa huyo alisema, wajumbe wanawake wamefikia 619, ambao wanachukua asilimia 27 ya idadi ya jumla, na kuongezeka kwa asilimia 2.8 kuliko Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama uliofanyika mwaka 2017.

Wajumbe 264 wanatoka makabila 40 madogomadogo.

Wajumbe hao watakaohudhuria mkutano mkuu wanatoka sekta mbalimbali za jamii, ofisi za mambo ya utawala za ngazi mbalimbali, pamoja na ofisi za Chama na serikali, idara za kiserikali, kampuni, na mashirika ya kiumma.

Wastani wa umri wa wajumbe hao ni miaka 52.2, na asilimia 59.7 ya wajumbe ni wenye umri wa chini ya miaka 55.

Asilimia 95.4 hivi ya wajumbe hao ni wenye shahada ya chuo au elimu ya juu zaidi. Zaidi ya nusu yao wana shahada ya uzamili.

Ofisa huyo alisema, kuna wajumbe 2,224 wanaochukua asilimia 96.9 ya idadi ya jumla ya wajumbe, ambao walijiunga na CPC tokea kuanza kwa mageuzi na kufungua mlango mwaka 1978.

Kutoka kuteuliwa, hadi kuthibitishwa na kuchaguliwa kwa wajumbe hao, mchakato huu mzima unafuata utaratibu kwa makini.

Matawi yote ya Chama kwenye mashina yalihamasishwa na kushiriki kwenye uchaguzi, na wastani wa washiriki wanachama walifikia asilimia 99.5.

Ofisa huyo alisema, hatua mbalimbali zilichukuliwa, zikiwemo kuanzisha jukwaa la kutoa ripoti na kuhamasisha vikundi vya kusimamia, ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika bila ya ufisadi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha