Mwaka mpya wa shule kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waathiriwa na mgogoro wa uasi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 28, 2022

Picha iliyopigwa Septemba 18, 2022 ikionyesha mtoto aliyekimbia makazi yake anapika kwenye jiko la muda katika makazi ya muda huko Rumangabo, Jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). (Xinhua/Alain Uaykani)

Tangu kuanza kwa mwaka mpya wa shule, shule zilizoko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimekumbwa na migogoro ya uasi bila kusita, huku madarasa yakikaliwa na wakimbizi waliokimbia makazi yao.

Wilaya ya Rumangabo ya Jimbo la Kivu Kaskazini, ambapo kwa sasa ni kiini cha mapigano ya kijeshi kati ya jeshi la serikali na jeshi la uasi wa Harakati za Machi 23 (M23), karibu watu 4,000 waliokimbia makazi wametawanyika katika shule tofauti, na kusababisha upunguza zaidi wa madarasa na rasilimali kuliko hapo kabla.

Marie Simire na watoto wake sita walikimbia kutoka Mji wa Bunagana ambao ulidhibitiwa na waasi, mume wake aliuawa kwa risasi zilizofyatuliwa ovyo akiwa njiani kuelekea nyumbani. Kama wenzake wengi kijijini, yeye na watoto wake walikimbia kwa siku kadhaa kwa kutembea kwa miguu na hatimaye wakakaa shuleni wakati wa likizo ya kiangazi.

“Nilifika hapa na watoto wangu kwa miezi kadhaa bila kuchukua chochote katika nyumba yetu huko Bunagana, sasa masomo yameanza tena lakini sina uwezo wa kuwapeleka watoto wangu darasani kutokana na ukosefu wa fedha na hali ngumu ya maisha." alieleza.

Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kiini cha Rumangabo, Jean-Baptiste Habyarimana, alibainisha hali halisi ya kuhuzunisha kwamba shule inaendeshwa kwa kupindukia uwezo wake, na idadi kubwa ya watu na watoto wao waliokimbia makazi yao imeleta tatizo kubwa kwa wakimbizi na watoto wanaosoma shuleni.

Mkuu wa eneo la makazi la wakimbizi huko Rumangabo, Katitima Justin, alisisitiza kuwa Watoto wengi katika eneo hili hawaendi shule. Kwa kuwa wanapenda kufanya kazi za ukataji kwa kuishi maisha. Tunasikitishwa na hali hii, ambayo inawezekana kuathiri mustakabali wa watoto hawa kwa muda mrefu."

Alipoulizwa na Shirika la Habari la Xinhua kuhusu hali ya sasa ya shule katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro kati ya jeshi ya serikali na waasi wa M23, kamanda mkuu wa Kivu Kaskazini Constant Ndima alikiri kwamba asilimia 70 hivi ya shule zimeathiriwa.

Kwa utawala wa kijeshi wa Jimbo la Kivu Kaskazini, suluhu madhubuti ni kurejesha amani katika sehemu hii ya nchi hiyo haraka iwezekanavyo ili kuwawezesha watu waliokimbia makazi yao kurudi nyumbani.

Lakini kwa Simire, kurudi nyumbani kunaonekana kama ni kufanya ndoto kwani maskani yake bado yamedhibitiwa najeshi la uasi. 

Picha iliyopigwa Septemba 18, 2022 ikionyesha watu waliokimbia makazi yao katika makazi ya muda huko Rumangabo, Jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). (Xinhua/Alain Uaykani)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha