Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC walichaguliwa kwa namna gani?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2022

Picha iliyopigwa Mei 22, 2020 ikionyesha bendera kwenye Uwanja wa Tian'anmen na sehemu ya juu ya Jumba la mikutano ya umma la Beijing. (Picha: Xinhua)

Wajumbe 2,296 watahudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) utakaofanyika hivi karibuni, na wajumbe hao walichaguliwa baada ya kupita mchakato wa kuwachagua kwa makini ipasavyo.

Wajumbe hao wanawakilisha wanachama zaidi ya milioni 96, walichaguliwa na idara 38, wajumbe hao watajadili na kuthibitisha ripoti ya kamati kuu ya 19 ya CPC na ripoti ya kamati kuu ya ukaguzi wa nidhamu ya chama kwenye Mkutano Mkuu utakaofanyika Beijing, ambao unafanyika kila baada ya miaka mitano.

Wajumbe hao watatoa maoni na matakwa ya wanachama na watu wa sekta mbalimbali, kujadilia na kuamua masuala makubwa ya chama, na kuchagua wajumbe wa awamu mpya wa kamati kuu ya CPC na wajumbe wa awamu mpya ya kamati kuu ya ukaguzi wa nidhamu ya chama.

Mjumbe Meng Xiangfei, ambaye ni mtaalamu mkuu wa sayansi katika utafiti na maendeleo ya programu za kompyuta yenye uwezo mkubwa alisema, “ hii ni fahari kwa wajumbe, lakini pia ni wajibu mkubwa sana.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha