Lugha Nyingine
Maafisa na wataalamu wa kigeni wautakia Mkutano wa 20 wa Taifa wa CPC mafanikio wakati wa maadhimisho ya Siku ya Taifa ya China
Balozi na ujumbe wa China katika mataifa na mashirika mbalimbali ya kimataifa zimefanya matukio ya kusherehekea mwaka wa 73 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China (PRC), ambapo maafisa na wataalam wa nchi za nje walitoa salamu zao za kuutakia mema Mkutano ujao wa 20 wa Taifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na kutazamia ushirikiano zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Tatiana Valovaya, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani Daren Tang, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani Guy Ryder, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani Ngozi Okonjo-Iweala na wakuu wengine wa mashirika ya kimataifa na wawakilishi wa kudumu wa nchi mbalimbali mjini Geneva wameeleza kufurahishwa kwao na mafanikio makubwa ambayo China imepata katika muongo mmoja uliopita, na kuutakia mafanikio Mkutano wa 20 wa Taifa wa CPC.
Wakitarajia kuendelea kuimarisha ushirikiano na China katika nyanja zao, wameeleza matarajio yao kuwa China itaendelea kuwa na nafasi muhimu katika mambo ya kimataifa na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa amani na maendeleo ya Dunia.
Rais wa Serbia Aleksandar Vucic ametoa salamu za maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Taifa ya China kwa watu wa China na kupongeza mchango uliotolewa na kampuni za China katika maendeleo ya uchumi wa Serbia.
“Serbia inajisikia fahari kuwa na urafiki wa chuma na China,” amesema Vucic, ambaye aliishukuru China kwa msaada na usaidizi wake wakati wa kipindi kigumu cha Serbia.
Vucic amesema anatumai Mkutano wa 20 wa Taifa wa CPC utafaulu na anatazamia kwa hamu ukurasa mpya wa ushirikiano wa hali ya juu kati ya nchi hizo mbili.
Akiutakia mafanikio mkutao huo, Valery Mitskevich, naibu mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi la Belarus, amesema anatumai kuwa nchi hizo mbili zitaimarisha ushirikiano wa Ukanda na Njia na kwamba makampuni zaidi ya China yatawekeza nchini Belarus.
Mmamosadinyana Molefe, katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Botswana, naye ametoa pongezi za dhati kwa maadhimisho ya miaka 73 tangu kuanzishwa kwa PRC na kuutakia Mkutano wa Taifa wa 20 wa CPC mafanikio.
Molefe ameishukuru China kwa uungaji mkono wake wa muda mrefu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Botswana na anaamini kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili utakua zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



