Mfugaji ajitolea kuboresha maisha kwa kupitia uhifadhi wa mbuga

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2022

Ting Bater akifanya kazi kwenye malisho yake katika Kijiji cha Sarultuya cha Abag, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, China, Septemba 8, 2022.(Xinhua/Liu Lei)

Ting Bater ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye alizaliwa mwaka 1955 katika Mji wa Hohhot wa Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China, na kuanza kufanya kazi katika Kijiji cha Sarultuya cha Abag Mwaka 1974.

Ting Bater akikagua zana katika Kijiji cha Sarultuya cha Abag, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China, Septemba 8, 2022.(Xinhua/Liu Lei)

Wakati huo, vyumba wafugaji wanavyoishi vilikuwa na mwanga mdogo na kitamba gandamizo chenye viraka. Familia nyingi hata hazikuwa na matandiko mazuri.

"Lakini wanakijiji walituandaa chakula chao kizuri zaidi," Ting alisema, tangu wakati huo nia yake ya kuwasaidia wafugaji kuishi maisha mazuri imeimarika.

Katika miaka hiyo, Ting alizoea haraka maisha ya ufugaji. Akiwa na umri wa miaka 21, alijiunga na Chama cha Kikomunisti cha China(CPC) na kuamua kubaki kwenye mbuga.

Mwaka 1993, Ting alianza kufanya kazi kama katibu wa Chama wa Kijiji cha Sarultuya.

Ting Bater akionesha picha ya mnyama pori aliyopiga katika malisho Septemba 8, 2022.(Xinhua/Liu Lei)

Kijiji cha Sarultuya kiko kwenye ukingo wa kaskazini-magharibi wa Hunshandake Sandland, kikiwa na mazingira tete ya kiikolojia. Kwa miaka mingi, Ting aliongoza kupanda miti katika maeneo yenye jangwa kubwa, akijenga hifadhi kadhaa wa miti.

"Kama akichukua uongozi, tunamfuata," mfugaji Yun Liang alisema. "Kwa sasa mapato ya familia yangu sasa imezidi yuani 300,000 (sawa na dola za kimarekani 42,000) kwa mwaka, na nyasi zinakua vizuri."

Ting Bater anatazama malisho yake katika Kijiji cha Sarultuya cha Abag, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China, Septemba 8, 2022.(Xinhua/Liu Lei)

Akitaja mpango wake wa siku za baadaye, Ting anasema ataendelea kufanya juhudi katika ulinzi wa ikolojia na ustawishaji wa vijijini. "Nitashirikiana na wafugaji kulinda mbuga, na kufanya juhudi kwa ajili ya maisha bora zaidi."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha