

Lugha Nyingine
Ajali ya kupinduka kwa meli kusini mwa Nigeria yasababisha vifo vya watu 76
Ikulu ya Nigeria ilitoa taarifa Tarehe 9 ikisema kuwa ajali ya kupinduka kwa kivuko juzijuzi katika Jimbo la Anambra, kusini mwa Nigeria ilisababisha vifo vya watu 76.
Taarifa ilisema kuwa tarehe 7 kivuko kilichobeba watu 85 kilipinduka kutokana na mafuriko kwenye mto katika eneo la Ogbaru la Jimbo la Anambra na kusababisha vifo vya watu 76. Rais wa Nigeria Buhari alitoa salamu za rambirambi kwa watu waliofariki dunia kwa ajali hiyo na kuitaka idara ya uokoaji kwenda kwa upesi eneo la ajali kuwatafuta na kuwaokoa watu wasiojulikana walipo.
Vyombo vya habari vya huko vilinukuu maneno ya ofisa mmoja wa Idara ya kukabiliana na hali ya dharura vikisema kuwa, katika eneo la ajali, mvua inanyesha kwa siku mfululizo, na maji ya mto yameongezeka sana, kivuko hicho kilipinduka wakati wa kuhamisha watu kwenye eneo lenye usalama.
Msimu wa mvua unaanza mwezi Aprili kila mwaka na kumalizika mwezi Oktoba katika sehemu mbalimbali nchini Nigeria.Wakati huo, kutokana na mvua kuendelea kunyesha, ni rahisi kusababisha mafuriko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma