

Lugha Nyingine
Zhang Jinmei: Kupanda Mikarafuu kwenye Uwanda wa Juu
![]() |
Zhang Jinmei (wa kati) pamoja na wenzake wakilinganisha tofauti kati ya maua ya mikarafuu mbili. (Zhang Long/Xinhua) |
Mji wa Xining wa Mkoa wa Qinghai una mwinuko wa mita 2300 hivi kutoka usawa wa bahari, ambapo hali ya hewa ya huko ni mbaya isiyofaa kukua kwa mimea na miti, lakini mikarafuu iliyopandwa huko inachukua asilimia 70 ya miti yote ya mji huo. Kila anapotembea kupita miti hiyo, mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kisayansi wa Misitu ya Mji wa Xining Bibi Zhang Jinmei hujivunia sana.
Maua ya Karafuu ni maua ya alama ya Mji wa Xining. Katika miaka ya 1990, mikarafuu ilipandwa kwenye sehemu mbalimbali mjini Xining, lakini mikarafuu iliyopandwa kwa mbegu bora ilikuwa kiasi kidogo , ambapo Zhang Jinmei alikaza nia ya kuotesha mbegu bora za mikarafuu inayofaa kukua kwenye nyanda za juu.
Baada ya kuhitimu kutoka Chuo cha Kilimo na Misitu cha Qinghai, Zhang Jinmei siku zote anajikitia katika kazi ya kuotesha na kuhifadhi mbegu bora za mikarafu adimu. Mwaka 2013, Zhang Jinmei aliteuliwa kufanya kazi kwenye Taasisi ya Utafiti wa Kisayansi wa Misitu ya Mji wa Xining, ambapo utafiti wake umewekwa mkazo katika kuotesha mbegu bora na kuhifadhi aina ya mikarafuu adimu.
Chini ya juhudi za Zhang Jinmei na wataalam wengine wa misitu siku hadi siku, hazina ya kwanza ya kitaifa ya mbegu za mikarafuu ya China ilianzishwa mjini Xining.
Zhang Jinmei amechaguliwa kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) mwaka huu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma