Lugha Nyingine
Maendeleo ya mtandao wa intaneti yasaidia uuzaji wa matufaha ya Uwanja wa Juu wa Manjano
![]() |
| Oktoba 10, 2022, mkulima mmoja akivuna matufaha katika shamba la matunda la Mji wa Yongxiang, Wilaya ya Luochuan, Mkoa wa Shanxi. |
Tofauti na wauzaji wa jadi wa matunda katika vijiji vya China, Zhang Xiuxiu alipofanya kazi alijiremba kila mara na kupenda kuvaa nguo za mtindo wa kisasa.
Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 33 anaendesha kampuni moja ya biashara ya mtandaoni inayouza matufaha katika Wilaya ya Luochuan, Mji wa Yan’an,ulioko Uwanja wa juu wa Majano, kaskazini magharibi mwa China.
Uwanja wa juu wa majano una mazingira mazuri ya asili kwa upandaji wa matufaha, na kuwezesha Wilaya ya Luochuan kuwa kituo mkuu cha matufaha nchini China.
Kampuni ya Zhang Xiuxiu imeuza matufaha zaidi ya kilo milioni 2.5 mwaka huu, na thamani ya mauzo ya jumla imezidi Yuani milioni 25 (sawa na dola za kimarekani milioni 3.52).
"Tunahitaji simu moja tu ya mkononi kwa kufanya kazi zote." Zhang Xiuxiu alisema.
Lakini, mwanzoni kuuza matufaha hakukuwa rahisi kwa Zhang Xiuxiu. Ni maendeleo ya kasi ya sekta ya mtandao wa intaneti ya China yanasaidia biashara ya mtandaoni ya Zhang Xiuxiu kupata mafanikio.
Naibu meya wa Mji wa Yan’an Wei Yan'an alisema, uenezi wa mfumo mpya na teknolojia sanifu ya upandaji, na uboreshaji wa miundombinu umesaidia kuongeza ubora wa matufaha, na kuweka msingi kwa uuzaji wa matufaha ya uwanda huo wa juu kupitia biashara ya mtandaoni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




