Lugha Nyingine
Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa vita, asema profesa akiunga mkono kauli ya Rais Xi Jinping alipofungua mkutano wa 20 wa CPC
(CRI Online) Oktoba 17, 2022

Mkuu wa Taasisi ya Sera za Afrika yenye makao yake makuu mjini Nairobi, Profesa Peter Kagwanja, amepongeza mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC unaoendelea hapa mjini Beijing.
Kagwanja amesema hotuba ya Rais Xi Jinping ya ufunguzi wa mkutano huo Jumapili imegusia maswala muhimu kwa China na dunia kama vile kushiriki kwenye uongozi wa kimataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha amesema dunia ya sasa haina nafasi ya vita lakini kinachohitajika ni mwongozo wa China wa kidiplomasia na mazungumzo katika kusuluhisha mizozo.
Profesa Kagwanja amezungumza na mwandishi wa CRI wa Nairobi Ronald Mutie.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



