Maendeleo Mapya ya China, Fursa Mpya kwa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 18, 2022

---Wataalamu wa kigeni watafsiri watoa maoni juu ya Ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha CPC

Wataalamu tisa wa kigeni wa lugha nane za Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiarabu, Kijerumani, Kijapan na Kilaos walikuwa wamealikwa kushiriki kwenye tafsiri za lugha mbalimbali za Ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China. Wataalamu hao ni watu waliopata mapema zaidi nakala za ripoti hiyo.

Mtaalamu wa lugha ya Kiingereza Bw. Sean Slattery anaona kuwa, ripoti hiyo si kama tu imeonesha matumaini makubwa ya ujenzi wa mambo ya kisasa, bali pia imetoa mpango kabambe kuhusu mambo halisi kwenye safari mpya ya China, na “inatupia macho siku za mbele”. Mtaalamu wa lugha ya Kijerumani V. Menzel alivutiwa sana na ripoti hiyo “yenye nguvu ya uhai”. Mtaalamu wa lugha ya Kilaos Pongtay Chaleunsouk alisema, kutokana na ripoti hiyo ameona mpango wa mambo ya kisasa unaoleta matumaini kwa nchi zinazoendelea, ambao hajauona mpango kama huo hapo kabla.

“Ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalumu wa China unafuatiliwa zaidi na watu”

Kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha CPC, wataalamu hao wa kigeni walipopata nakala za ripoti hiyo walijikita mara moja kwenye kazi hii yenye “changamoto” na “wanayoona majivuno”.

Wataalam kadhaa walipohojiwa na waandishi wa habari wa Shirika la habari la China Xinhua, walisema, “Ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalum wa China” katika ripoti aliyotoa Xi Jinping katika mkutano mkuu, unafuatiliwa zaidi na watu, na walipotafsiri walifikiria kwa makini zaidi namna ya kueleza ipasavyo maana yake halisi.

Mtaalamu wa lugha ya Kiingereza Sean mwenye umri wa miaka 33 alipotaja sifa tano za ujenzi wa mambo ya kisasa ya China alisema, “sifa hizo ni tofauti na zile za ujenzi wa mambo ya kisasa unayofanyika duniani, na zina umuhimu mkubwa”.

Mtaalamu wa lugha ya Kiarabu kutoka Sudan Yahia Mustafa anakubaliana na maoni hayo. Alisema, “ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalum wa China ni tofauti na ujenzi wa magharibi uliowekwa kwenye msingi wa kufanya unyang’anyi, vita na kumwaga damu. Ujenzi huo wa mambo ya kisasa ya China unafanyika kwenye msingi wa kujitawala na kujiamulia, kufuata njia ya amani na kufanya ushirikiano wa kimataifa, na umeleta chaguo jipya kwa binadamu wote.

“Wananchi, mazingira, amani”. Mtaalamu kutoka Ufaransa Peggy ametoa maneno matatu muhimu yanayomfualitia zaidi.Wataalam wa kigeni na wenzao wa China walifanya majadiliano mara kwa Mara katika kazi ya tafsiri, hatimaye walipata tafsiri kuhusu “Ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalum wa China”, wanayoona ni ya sahihi zaidi, huku wakielewa kwa kina undani wa maana ya maneno hayo, walisema “China imevumbua hali mpya ya aina moja ya ustaarabu wa binadamu.”

Miaka 10 ya zama mpya ina “umuhimu wa kufungua ukurasa mpya”

Ripoti iliyotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha CPC imefanya majumuisho kwa pande zote mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka 10 katika zama mpya. Kwa wataalamu hao wa kigeni, maelezo yote ya ripoti hiyo yanaweza kuwakumbusha mambo waliyoshuhudia wenyewe.

Mtaalamu wa lugha ya Kihispania Francisco J. Ayllon amefanya kazi na kuishi nchini China kwa miaka 18, alisema, anashangazwa na mafanikio ya China katika kuondoa umaskini. China ilipata ushindi katika kupambana na umaskini, ambayo ni mapambano makubwa zaidi katika historia ya binadamu, ikawafanya wakulima vijijini China karibu milioni 100 waondokane na umaskini katika muda usiofikia miaka 10, “hii imetoa mchango mkubwa kwa ajili ya mambo ya kuondoa umaskini duniani”.

Mtalamu wa lugha ya Kirusi K.Angelina ameona kuwa, sasa wachina wanaweza kupata siku nyingi za anga buluu, maji safi, mashamba yanayofaa kulima, na magari yanayotumia nishati mpya yameongeza zaidi pia.

Mtaalamu wa lugha ya Kijapan Taguchi Nao alipotafsiri ripoti hiyo aliguswa sana na maelezo yake kuhusu huduma za jamii, kazi ya afya nchini China, na kukabiliana na hali ya kuongezeka kwa idadi ya wazee, alisema, “sisi pia tunahitaji sana uzoefu huo katika kazi ya maendeleo”.

Mjerumani V.Menzel ameishi nchini China kwa miaka 11. Mbali na kufurahi na kupata urahisi katika kulipa malipo ya matumizi kwa simu ya mikononi, kupanda baiskeli za matumizi ya kiumma, na kununua vitu kwenye mtandao wa intaneti, anajionea zaidi “China imeonekana imani yake ya nchi kubwa, ikiwemo pamoja na imani yake ya utamaduni wa China.” Katika wakati wa kutafsiri ripoti hiyo, mtaalmu wa lugha ya Kilaus alitazama “Utoaji Mafunzo Kwenye Anga ya Juu” uliooneshwa kwenye televisheni nchini China hivi karibuni.

Alisema, kwa kulinganishwa na baadhi ya nchi za magharibi, China imechelewa kupiga hatua katika kuendeleza mambo ya safari kwenye anga ya juu, lakini hivi China imekuwa kwenye safu ya mbele katika sekta hiyo duniani, na imejikita katika kufanya maingiliano na ushirikiano wa kimataifa.”

“Kusoma na kuelewa hali halisi ya kweli ya Chama cha Kikomunisti cha China”

Wataalamu walioshiriki kwenye kazi ya kutafsiri ripoti ya mkutano mkuu wa Chama walisema, kuelewa maana ya lugha ya Kichina hakutosha kabisa katika kazi ya tafsiri, kwanza lazima kusoma na kuelewa hali halisi ya kweli ya Chama cha Kikomunisti cha China, na kuelewa kwa kina kuhusu historia ya chama hicho na falsafa yake ya utawala wa nchi.

Chama cha Kikomunisti cha China kinachukua kazi ya kuleta manufaa kwa wananchi kuwa ni mafanikio makubwa zaidi. Katika ripoti iliyotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa chama hicho, maneno ya kisiasa yenye umaalum wa China kama vile “Uungaji mkono wa watu ni siasa kuu”, “Wananchi Juu Zaidi”, “Mito na milima ni watu, na watu ni mito na milima” yamewapa kumbukumbu zaidi. “Mawazo na maneno hayo yameonesha kuwa, Chama cha Kikomunisti cha China kimeweka wananchi kwenye hadhi ya juu zaidi ”, alisema mtaalamu wa lugha ya Kingereza Sean Slattery.

Mtaalam wa lugha ya Kiarabu Yahia Mustafa anakumbuka kuwa, ripoti iliyotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama cha CPC ilisema “kufanya juhudi kubwa ili kupata ushindi wa mwisho katika kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote”. Chama cha Kikomunisti cha China kimetimiza ahadi yake kwa mpango uliowekwa. Mtaalamu huyu alisema, Chama cha Kikomunsti cha China kinawaongoza wananchi wake bilioni 1.4 katika kupigania kujenga kikamilifu nchi yenye mambo ya kisasa ya kijamaa, na anaamini kuwa bila shaka Chama cha CPC kitaweza kutimiza ahadi yake hiyo.

Chama cha Kikomunisti cha China kimekuwa na wanachama zaidi ya milioni 96, kimekuwa chama kinachofuata falsafa ya Umarx chenye nguvu kubwa ya mshikamano wa kisiasa na kuwa na imani ya kujiendeleza.

Mtaalamu wa lugha ya Kijerumani V. Menzel alipomwelezea mwandishi habari alisema, amepata kumbukumbu zaidi kuhusu Chama cha CPC kimeahidi kuwa kitashikilia thamani ya kimsingi na mila na desturi za utamaduni, huku kikithubutu kufanya uvumbuzi, kuendelea kufungulia mlango na kujipatia maendeleo.”

Mtaalamu wa lugha ya Kifaransa Peggy alisema “Chama cha Kikomunisti cha China ni chama chenye uwezo mkubwa wa kufanya utafiti, kuchukua vitendo, kwenda na wakati na kufanya uvumbuzi.”

China inayowajibika italeta manufaa kwa dunia

Ripoti hiyo imesema, China itakamilisha kimsingi ujenzi wa mambo ya kisasa ya kijamaa kuanzia mwaka 2020 hadi 2035, na kuanzia mwaka 2035 hadi katikati ya karne hii kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu ya mambo ya kisasa ya kijamaa ya ustawi, demokrasia, ustaarabu, maafikiano na yenye sura mpya nzuri.

Mtaalamu wa lugha ya Kijerumani V. Menzel ameona kuwa, “kufanya uvumbuzi” ni maneno yaliyotajwa mara kwa mara kwenye ripoti hiyo, anaona hii ni fursa ya kufanya ushirikiano na kupata maendeleo zaidi kwa Ujerumani inayotilia maanani pia uvumbuzi. Aidha, ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ni mali ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

Mtaalamu wa lugha ya Kiarabu Yahia Mastafa alisema, ana matarajio makubwa juu ya ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu katika sekta za uchumi na biashara, na ujenzi wa miundombinu.

Mtaalamu wa lugha ya Kiingereza Sean Slattery alisema, ripoti hiyo imeonesha kuwa China inahitaji amani, inatarajia amani, na inapenda kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani ya dunia.

Dunia imesimama tena kwenye njia panda ya kihistoria. China inasimama kithabiti kwenye upande wa usahihi wa kihistoria, kwenye upande wa maendeleo ya binadamu. Ripoti iliyotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China inaeneza busara ya China, mpango wa China na wajibu wa China.

Bw. Yahia alisema, “Baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, China itakaribisha maendeleo mapya katika mambo ya kisasa. Mimi nina matumaini ya pamoja na watu wa China katika kushuhudia mchakato huo mkubwa wa kihistoria”.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha