

Lugha Nyingine
CPC chapanga mikakati zaidi kuelekea safari ya ustawi wa pamoja kwa watu wote
BEIJING - Kwa wengi, mmea wa moss si chochote ila mmea mdogo mdogo unaokua katika sehemu zisizo na thamani zenye unyevunyevu, lakini kwa wanakijiji katika mji mdogo wa milimani wa Maoyang nchini China, mmea huu umeleta pesa na kuwaondoa kwenye umaskini na kuwaweka kwenye safari ya kupata utajiri zaidi.
Mji huo wa mbali uko katika tarafa moja kati ya tarafa zenye maendeleo duni zaidi katika Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, mkoa wenye nguvu kubwa kiuchumi na wa majaribio katika kufikia ustawi wa pamoja wa watu wote wa China.
Kwa kuzingatia rasilimali zake za asili, mji huo mdogo umekuza tasnia inayokua ya upandaji wa mimea ya moss na kuuza bidhaa zinazohusiana nayo. Mwaka jana, biashara ya moss ilizalisha zaidi ya yuan milioni 17 (kama dola milioni 2.4 za Kimarekani) kwa wanakijiji.
Mwanakijiji akipanga bidhaa zinazotokana na mimea ya moss zilizoagizwa mtandaoni kwa ajili ya kupelekwa katika Mji mdogo wa Maoyang wa Mji wa Lishui, Mkoa wa Zhejiang nchini China, Februari 24, 2021. (Xinhua/Jiang Han)
Miongozo mipya
Maendeleo ya mambo ya kisasa ya China yanalenga kuleta ustawi wa pamoja kwa Wachina wote, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Xi Jinping, katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.
Ripoti hiyo iliorodhesha mkakati mzima na hatua za ujenzi wa China ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa kwenye sekta zote katika kipindi cha miaka mitano ijayo na zaidi, ikielezea hatua za kukuza na kushiriki ipasavyo maendeleo ya nchi.
Watalii wakicheza dansi katika Kijiji cha Sanping cha Mji wa Zhongyuan katika Tarafa ya Jing'an, Mkoa wa Jiangxi nchini China, Julai 27, 2022. Sanping, kijiji kilichokuwa na umaskini, sasa kimekuwa kituo maarufu cha utalii wa mapumziko wakati wa majira ya joto. (Xinhua/Wan Xiang)
Kupanua na kuchangia matunda ya maendeleo
Ikiwa ni hitaji muhimu la ujamaa na sifa maalumu za maendeleo ya kisasa ya China, ustawi wa pamoja kwa wote unahusu zaidi utajiri unaoshikiliwa na kila mtu."Kwanza tutaufanya utajiri kupanuka na kuwa mkubwa zaidi, na kisha kuugawanya ipasavyo kupitia mipangilio ya kitaasisi inayofaa," Xi alisema katika hotuba maalum kwenye mkutano wa mtandaoni wa Jukwaa la Uchumi la Dunia la Mwaka 2022 uliofanyika Mwezi Januari.
Dira hii ilipata uangalizi maalum wa ndani na kimataifa Mwaka 2020, na malengo yake yamefafanuliwa katika mpango wa 14 wa miaka mitano wa maendeleo ya taifa ya kiuchumi na kijamii na malengo ya dira ya muda mrefu hadi Mwaka 2035.
Wakazi wenyeji wakipiga picha mbele ya nyumba yao mpya katika Mji wa Gurum wa Lhasa, Mkoa unaojiendesha wa Tibet nchini China, Aprili 2, 2020. (Xinhua/Zhan Yan)
Juhudi kubwa katika pande zote
Juhudi za pamoja kote nchini China zinafanikisha hatua kwa hatua lengo la ustawi wa pamoja kwa kutumia maarifa ya zamani na kuibua njia mpya.
Kama ilivyo kwa juhudi nyingine nyingi za China, msukumo wa ustawi wa pamoja una waanzilishi wake. Mwaka 2021, China ilitoa mwongozo wa kujenga Mkoa wa Zhejiang kuwa eneo la kielelezo na la mfano ili kufikia ustawi wa pamoja ifikapo Mwaka 2035.
Ili kupunguza pengo kati ya maeneo yake tajiri ya pwani na maeneo ya milimani yasiyo na utajiri, Zhejiang imeimarisha ushirikiano kati yao kupitia msururu wa mipango ya kuoanisha.
Mipango na sera za Mkoa wa Zhejiang sasa zinatekelezwa katika mikoa na maeneo yote ya China kwa ajili ya kufikia ustawi wa pamoja kwa wachina wote.
Picha iliyopigwa kutoka angani ikionyesha wafanyakazi wakifanya usafi wa kawaida kando ya mto katika Kijiji cha Dongheng cha Tarafa ya Deqing katika Mji wa Huzhou, Mkoa wa Zhejiang nchini China, Aprili 12, 2022. (Picha na Wang Zheng/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma