Lugha Nyingine
China kuendelea kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja

Ma Zhaoxu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing, China, Oktoba 20, 2022. Kituo cha waandishi wa habari cha Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) siku ya Alhamisi kiliandaa mkutano wa waandishi wa habari wenye mada isemayo "Chini ya Mwongozo wa Fikra za Xi Jinping juu ya Diplomasia, Kusonga Mbele na Kujitahidi Kujenga Msingi Mpya wa Diplomasia ya nchi kubwa yenye Umaalumu wa China". Shen Beili, Naibu Waziri wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya CPC, pia alihudhuria mkutano huo na waandishi wa habari. (Xinhua/Chen Jianli)
BEIJING - China itahimiza kwa vitendo madhubuti ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na kufanya kazi ili kufanya mfumo wa usimamizi wa kimataifa kuwa wenye haki na usawa zaidi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Ma Zhaoxu amesema Alhamisi.
Ma ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China.
“Juhudi za kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja zimepata maendeleo makubwa katika nyanja na masuala mbalimbali,” amesema.
Ameeleza kuwa Mpango wa Ukanda Mmoja, Njia Moja unaopendekezwa na China umekuwa jukwaa lenye maslahi ya kiumma ya kimataifa na jukwaa muhimu la ushirikiano wa kimataifa, na kuongeza kuwa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia na Pendekezo la Usalama wa Dunia kwa pamoja yameleta msukumo mpya kwa amani na maendeleo ya Dunia.
“China iko imara katika kulinda mfumo wa kimataifa huku Umoja wa Mataifa (UN) ukiwa ndiyo msingi wake, utaratibu wa kimataifa unaoungwa mkono na sheria za kimataifa, na kanuni za msingi zinazosimamia uhusiano wa kimataifa kwa kuzingatia madhumuni na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa,” Ma amesema.
Ameweka bayana kuwa ubinadamu unakabiliwa na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa, na umwamba na uonevu unaofanywa na baadhi ya nchi ni tishio kubwa kwa utaratibu wa Dunia. "Dunia iliyogawanyika haina faida kwa mtu yeyote, na makabiliano ya kambi yatasababisha mwisho mbaya."
Amesema China itafanya utafiki juu ya maendeleo yake huku ikilinda kwa uthabiti amani na maendeleo ya Dunia, na kuhimiza vyema amani na maendeleo ya Dunia kupitia maendeleo yake yenyewe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



