Lugha Nyingine
Nchi 181 duniani sasa zina uhusiano wa kidiplomasia na China

Kituo cha waandishi wa habari cha Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimeandaa mkutano na waandishi wa habari uliopewa mada isemayo "Chini ya Mwongozo wa Fikra ya Xi Jinping juu ya Diplomasia, Kusonga Mbele na Kujitahidi Kujenga Msingi Mpya wa Diplomasia ya nchi kubwa yenye Umaalumu wa China" hapa Beijing, China, Oktoba 20, 2022. Shen Beili, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Mambo ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya CPC, na Ma Zhaoxu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, walihudhuria mkutano huo na waandishi wa habari. (Xinhua/Chen Jianli)
BEIJING - Jumla ya nchi 181 duniani zimeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China, ikiwa ni idadi iliyoongezeka kutoka nchi 172 miaka 10 iliyopita, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Ma Zhaoxu amesema hapa Alhamisi, huku akipongeza huduma za kidiplomasia za China katika muongo mmoja uliopita.
Akizungumza na waandishi wa habari kando ya Mkutano Mkuu wa 20 unaoendelea wa Chama cha Kikomunisti cha China, Ma amesema hadi sasa China imeanzisha uhusiano wa wenzi na nchi na mashirika ya kikanda duniani 113 kutoka 41 katika muongo mmoja uliopita.
Ma amesema China imepiga hatua mbele katika kujenga ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Russia wa zama mpya, imependekeza kanuni tatu za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kufanya ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Marekani na kutetea uhusiano wa wenzi kati ya China na Umoja wa Ulaya ulio wa amani, ukuaji wa uchumi, mageuzi na ustaarabu.
“Pia China imeimarisha uungaji mkono wa kimkakati kutoka nchi jirani, na kuongeza mshikamano na ushirikiano wa karibu na nchi nyingine zinazoendelea” amesema.
Mamlaka ya nchi , usalama na maslahi ya maendeleo ya China yamelindwa kwa nguvu zote katika mchakato huo, Ma amesema, huku akiongeza kuwa China sasa imeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi tisa ambazo hapo awali zilikuwa na kile kinachoitwa "uhusiano wa kidiplomasia" na eneo la Taiwan la China. Amesema kuwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, juhudi za kidiplomasia za China zimeimarisha uungaji mkono wa kimataifa kwa kanuni ya kuwepo kwa China moja, zimezuia uingiliaji kati wa nguvu ya nje katika mambo ya Hong Kong, kuzuia mashambulizi na kashfa za nguvu inayoipinga China, na kulinda maslahi na heshima ya nchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



